Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKOA
wa Pwani unatarajia kuchanja watoto wote wenye umri chini ya miaka
mitano wapatao zaidi ya 263,990 ili kuwakinga na ugonjwa wa polio kwa
utoaji wa matone.
Hayo
yalisemwa Mjini Kibaha na Mganga Mkuu wa Mkoa huo,Dkt. Gunini Kamba
wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kampeni ya utoaji wa
matone ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio.
Kamba
alisema kuwa kampeni hiyo ya utoaji matone itakuwa ya siku nne ambapo
lengo ni kuhakikisha watoto wote wanaostahili kupata chanjo wanapatiwa
chanjo hiyo kwa wale wote wenye umri chini ya miaka mitano .
"Mkoa
ulifanya vizuri katika awamu ya pili kwa Kuvuka lengo la Uchanjaji kwa
kufikia jumla ya watoto walio na umri chini ya miaka mitano 263,851
ambayo ni asilimia 131.2 ya walengwa wote na hivyo wanatarajia kufanya
vizuri zaidi katika awamu hii ya tatu."
"Naomba
nitoe rai kwa viongozi na watendaji wote wa Serikali, vyama vya Siasa,
Dini, Taasisi na Wadau wote katika kuhakikisha tunashirikiana kikamilifu
na kuhakikisha jamii yetu hususani wazazi na walezi wa watoto wanapata
taarifa sahihi juu ya zoezi hili na umuhimu wake kwa afya za watoto
wetu,"alisema Kamba.
Nae
mratibu wa chanjo Mkoani hapo , Abbas Hincha alisema katika kuhakikisha
kila mtoto anafikiwa timu za uchanjaji zitapita nyumba kwa nyumba na
sehemu yoyote ile walipo watoto sokoni, shule za chekechea, nyumba za
ibada na Kauli mbiu inasema kila tone la chanjo ya polio litaiweka
Tanzania salama dhidi ya ugonjwa wa kupooza.
Alieleza,
chanjo hiyo siyo mara ya kwanza kutolewa hapa nchini hivyo wazazi
wahakikishe watoto waliolengwa wanafikiwa na chanjo hiyo .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...