Na. Damian Kunambi, Njombe
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani Benki ya CRDB tawi la Ludewa imeadhimisha siku hii kwa kula keki pamoja nabaadhi ya wateja wao waliofika katika tawi hilo kwajili ya kupata huduma huku wakipongeza viongozi wa wilaya hiyo na wananchi kwa kupokea vyema huduma hiyo.
Akizungumza katika sherehe hiyo fupi iliyofanyika katika ofisi za benki hiyo Kaimu Meneja wa tawi hilo Daniel Maruchu amesema wameona ni vyema kusherehekea siku hiyo na wateja wao kwani tawi hilo limefunguliwa hivi karibuni na kumekuwa na mwitikio mzuri wa watu.
"Tunawashukuru sana wananchi wa Ludewa kwa kuipokea vizuri benki yetu na pia viongozi mbalimbali kwani tumekuwa tukishirikiana nao kwa ukaribu katika huduma zetu pamoja na shughuli mbalimbali za kijamii". Amesema Maruchu.
Amesema benki hiyo imejipanga kuboresha zaidi huduma zake na kutoka mikopo yenye gharama nafuu ili kuwawezesha wateja wake kupata mikopo yenye unafuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...