Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amesema darala la Kinyasungwi-Godegode lenye urefu wa mita 154, linalounganisha jimbo la Mpwapwa na Kibakwe mkoani Dodoma litaanza kujengwa ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kukagua barabara ya Mpwapwa-Gulwe- Kibakwe yenye urefu wa Km 48.1 Eng. Kasekenya amesema Serikali inatambua umuhimu wa daraja Kinyasungwi-Godegode katika barabara hiyo kiuchumi na kijamii hivyo ujenzi wa daraja hilo utaendana na ujenzi wa barabara unganishi za lami zenye urefu wa Kilomita 6.

“Barabara hii ni muhimu kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na ni kiunganishi kizuri cha mikoa ya Dodoma-Morogoro hadi Dar es Salaam hivyo kukamilika kwake kutaibua fursa za maendeleo kwa wakazi wa Wilaya ya Mpwapwa”, amesema Eng. Kasekenya.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kasekenya amemtaka mkandarasi Mtwivila Traders anayejenga madaraja madogo katika barabara ya Kongwa-Mpwapwa yenye urefu wa KM 49.19 na mkandarasi Technics Constructions Group anayejenga daraja la Mpwapwa kuhakikisha yanakamilika kabla ya mvua za masika ili kuepusha athari katika madaraja hayo.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Dodoma Eng. Salehe Juma amemhakikishia Naibu Waziri Kasekenya kuwa wamejipanga vizuri na ujenzi wa madaraja hayo na barabara unganishi utakamilika kwa wakati na ubora uliokusudiwa.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Josephat Maganga amesema kukamilika kwa madaraja hayo kutaondoa adha wanayoipata wananchi hususan wakati wa mvua kubwa na kuboresha ustawi wa maisha ya jamii katika eneo hilo.Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma, Mhe. Josephat Maganga (kulia) akimkabidhi Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya Taarifa ya utekelezaji wa miradi iliyopo wilayani kwake ambayo inasimamiwa na Wakala wa Brabara Tanzania (TANROADS) mkoani humo.Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (Wa kwanza kushoto) akitoka kukagua ujenzi wa daraja wilayani Mpwawa, jijiniDodoma. Daraja hilo linaunganisha wilaya hiyo na wilaya ya Kongwa.Mafundi wa Kampuni ya kikandarasi ya Technics Constructions wakiendelea na ujenzi wa daraja dogo Wilayani Mpwapwa, jijini Dodoma.Muonekano wa juu wa daraja dogo linalojengwa na Kampuni ya kikandarasi ya Technics wilayani Mpwapwa, jijini Dodoma. Daraja hilo linaunganisha vijijivilivyopo wilayani humo katika bonde la Shaaban Robert

PICHA NA WUU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...