Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu anatarajiwa kuwa Mgeni
rasmi katika hafla ya kutangaza matokea ya Sensa ya watu na Makazi
mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.
Akizungumza
Jijini Dar es salaam leo Oktoba 12,2022 Kamisaa wa Sensa Anna Makinda amesema
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikamilisha rasmi zoezi la
kuhesabu watu,Majengo pamoja na Anwani za Makazi kutokana na hamasa ya
wananchi ambayo wameionyesha na kukamilisha zoezi hilo Kwa wepesi.
Makinda
amefafanua zaidi kuwa Sensa ya mwaka huu imetumia teknolojia ya Hali ya
juu iliyohusisha matumizi ya vishikwambi katika awamu zote za
utekelezaji na kuongeza ubora wa takwimu zilizokusanywa.
"Tangu
kukamilika Kwa zoezi la kuhesabu watu,wataalamu wamekuwa wakiendelea na
kazi ya Uchakataji wa taarifa zilizokusanywa Ili kupata matokea
mbalimbali ya sensa hiyo."
Aidha,Kamisaa
ameeleza kuwa Serikali inatoa pongezi na kuwashukuru wananchi wote kwa
namna walivyojitoa kuhakikisha Sensa ya watu na Makazi Kwa mwaka huu
linafanikiwa.
"Serikali
itaendelea kuwahusisha wanahabari katika kuelimisha na kuhamasisha umma
kuhusu matumizi ya matokea ya sensa katika mipango jumuishi Kwa
Maendeleo endelevu ya Taifa."
Kamisaa wa zoezi la Sensa Anna Makinda akizungumza na waandishi
wahabari Leo Jijini Dar es salaam katika ofisi za takwimu na kutangaza
rasmi kuwa Mgeni rasmi wa uzinduzi wa matokea ya Sensa anatarajiwa kuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan uzinduzi
ambao utafanyika mwishoni mwa mwezi octoba mwaka huu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...