Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Oktoba 3, 2022 amewasili mjini Istanbul-Uturuki kwa ajili ya ziara ya kikazi na pia kufuatilia Mashindano ya Kombe la Dunia kwa watu wenye ulemavu yanayoendelea nchini humo.

Mhe. Mchengerwa amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Lt. Gen. Yacoub Mohamed na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi ambaye alitangulia.

Akizungumza mara baada ya kuwasilili ameipongeza timu ya Tembo Warriors kwa kuifunga Uzbekistan goli 2-0 kwenye mechi iliyopigwa leo Oktoba 3, 2022 katika uwanja wa TFF RIVA.

“Nawapongeza Tembo Warriors na watanzania wote waishio nchini Uturuki kwa kuleta hamasa kubwa katika mashindano haya. Tanzania inaweza na tukiacha uvivu tutafika mbali na ushindi huu ni wa watanzania wote” alisema Mhe. Waziri Mchengerwa.

Aidha amempongeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi kwa kuhakikisha timu inakuwa sawa kisaikolojia na pia kuhamasisha hamasa katika mechi zote za mashindano.

“Wizara yetu haina jambo dogo, sisi kila jambo ni kubwa na tutahakikisha Tanzania haitobaki nyuma katika mchezo wowote ule” alisema.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...