Na.Ashura Mohamed,Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha Mhandisi Richard Ruyango amesema kuwa serikali itaendelea kutengeneza mazingira mazuri wilayani humo ili kuwawezesha wawekezaji kuendelea kufanya kazi katika mazingira wezeshi.

Alisema kuwa ni vema wawekezaji wakaendelea kuwekeza katika wilaya hiyo kwa kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuwapa,kipaumbele ili waweze kufanya shughuli zao Vizuri.

Ameyasema hayo wakati wa Mahafali ya Tatu ya Kidato Cha nne,darasa la Saba na watoto wadogo wanaoingia darasa la kwanza (Kindergarten),katika shule ya Turkish  Maarif iliyopo eneo la Ngaramtoni wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.

"Wawekezaji kama hawa  wanatusaidia Sisi watanzania wametoka nchini mwao,kuja kuendeleza watoto wetu wa kitanzania na umeona hapa kuwa kuna mambo mengi mazuri wanafanya kwa vijana hawa wa kitanzania,Vipaji vikubwa lakini kitu kizuri hawajaacha kufundisha Mila na desturi za kitanzania tumeona hawa vijana wadogo"Alisema Mhandisi Richard

Aidha alitumia wasaa huo kuwapongeza walimu kwa jitihada kubwa wanazozifanya kwa kuwalea watoto kimaadili na kitaluma kuanzia wakiwa wadogo mpaka Sasa wanapohitimu  masomo Yao.

Pia aliwasisitiza wazazi kuendelea kuwasaidia vijana na kusimamia,maadili kwa kuwa wazazi ni wana asilimia 50 ya kuhakikisha kuwa Taifa linapata vijana ambao wanauzalendo na weledi wa kutosha.

Nae Mkuu wa shule ya Msingi Turkish Bw.Raphael Sabaya alisema kuwa ni vema jamii ikabadili mtizamo kwa kuendeleza vipaji vya watoto ili kuondoa dhana kuwa elimu ya darasani inaweza kuwatoa kimaisha.

Bw.Sabaya alisema kuwa sio lazima Mtoto ategemee elimu ya darasanj,bali elimu ya vitendo inaweza kusaidia kujiajiri na kuondokana na changamoto ya ajira iliyopo nchini na duniani kwa Ujumla.

Jumla ya wanafunzi 33 wamehitimu kidato Cha nne,31 darasa la saba na watoto wadogo (kindergarten) 28.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha mhandisi Richard Ruyango akitoa vyeti kwa  mmoja wa wahitimu wa darasa la Saba,Shuleni Turkish Maarif.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...