Na Mwandishi wetu, Simanjiro
UCHAGUZI
wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa wanawake wa CCM Tanzania UWT
Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara unatarajiwa kurudiwa upya Oktoba 15.
Katibu wa UWT wilaya ya Simanjiro, Leokadia Fisoo amesema uchaguzi huo unatarajiwa kurudiwa tena jumamosi ijayo ya Oktoba 15.
Fissoo
amesema uchaguzi huo unatarajiwa kurudiwa mara baada ya mmoja kati ya
wagombea wa nafasi hiyo kukata rufaa ngazi ya UWT Taifa.
Amesema
malalamiko ya mgombea huyo yameonekana ni sahihi hivyo uchaguzi huo
utarudiwa upya kwenye nafasi moja ya Mwenyekiti wa UWT wilaya ya
Simanjiro.
"Uchaguzi
utarudiwa jumamosi ijayo na nimeshawapa taarifa wajumbe wa kata husika
na wajumbe wa wilaya juu ya kurudiwa kwa uchaguzi huo," amesema Fissoo.
Amewataja
watakaogombea nafasi hiyo ni wale waliopitishwa na halmashauri Kuu ya
CCM mkoa wa Manyara ambao ni Agnes Brown, Anna Shinini, Naomi Edward na
Rehema Yohana.
Awali,
uchaguzi wa UWT wilaya ya Simanjiro ulifanyika Septemba 24 mwaka huu
ambapo kwa nafasi hiyo ya Mwenyekiti ililazimika kurudiwa mara mbili.
Katika
uchaguzi huo matokeo yalikuwa Anna Shinini aliongoza kwa kupata kura
97, Agnes Brown 86, Naomi Edward 10 na Rehema Yohana 2.
Hata
hivyo ikabidi uchaguzi huo urudiwe tena kutoka a na mshindi kutokupata
zaidi ya asilimia 50 na matokeo yakawa Agnes kura 99 na Anna kura 96.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...