Na John Walter-Manyara
Baadhi ya wananchi wanaoishi maeneo ya mpaka wa mkoa wa Manyara na Singida wamesema kwa sasa wanaishi kwa hofu kubwa kutokana na kufanyiwa vitendo visivyo vya kiungwana vya kuchomwa moto nyumba zao na kuuawa mifugo.
Wananchi hao wanaoishi katika vijiji vya Kaza moyo na Gorimba kata ya Lalaji wilaya ya Hanang wamesema mara kadhaa wanavamiwa na kuambiwa eneo hilo ni la mkoa wa Singida hivyo wanapaswa kuhama haraka iwezekanavyo.
Aidha wananchi hao wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro huo kwa kubainisha mpaka kati ya mkoa wa Singida na Manyara kwa lengo la kuwasaidia wananchi kuondokana na kero hiyo iliyowasumbua kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Kamishna wa ardhi Msaidizi Leornard Msafiri amesema kama mkoa wanatambua juu ya mgogoro huo na tayari wapo kwenye mchakato wa kuweka alama za kudumu katika maeneo hayo na amewasihi wananchi kuwa watulivu wakati mchakato huo unaendelea kufanywa na serikali.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...