Na Jackson Gaspaly wa Michuzi TV, Morogoro


Watu 5 wamefariki dunia papo papo Mikumi Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro katika ajali iliyohusisha gari ndogo maarufu kama "IT"  iliyokuwa ikitokea  Bandarini Jijini Dar-es-salaam kuelekea  mpakani Tunduma  baada ya   kugongana  uso kwa uso na gari kubwa la mafuta  aina ya Benzi  iliyokuwa ikitokea Mkoani Iringa kuelekea Mkoani Morogoro.


Akithibitisha ajali hiyo, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Morogoro FORTUNATUS MUSILIMU amesema ajali hiyo iliyotokea majira ya  usiku wa kuamkia Jumatatu eneo la  IYOVI wilayani Kilosa  Mkoani Morogoro  katika barabara kuu ya  Morogoro-Iringa na kusema imesababishwa na  uzembe wa dereva wa wa gari ndogo ambaye inasemekana alikuwa akiendesha kwa kasi na gari likamshinda katika kona na kuvamia lori hilo.



Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Morogoro FORTUNATUS MUSILIMU akikagua lori lililohusika na ajali hiyo.


Gari ndogo maarufu kama "IT"  iliyokuwa ikitokea  Bandarini Jijini Dar-es-salaam kuelekea  mpakani Tunduma baada ya ajali hiyo.




Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Morogoro FORTUNATUS MUSILIMU akiwasilisha taarifa ya ajali hiyo kwa wanahabari  eneo la tukio.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...