Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Ningeweza kukuita nilipo ukaja au kunyanyua simu yangu kukwambia haya nilyoandika, lakini nimechagua ‘Open Letter’ ibaki kumbukumbu hata kwa Wavulana wenzio wenye ndoto kama zako.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya Kijamii, Haji Manara ameandika hivi…”Nimeangalia kila sekunde uliyochezea Yanga SC, naiona mbali kesho yako Kwa jinsi unavyocheza kikubwa, ‘touch’ yako kwenye ‘scoring’ ‘dribbling’ yako, ‘accuracy’ uliyojaaliwa, ‘control ball’ ya haja, ‘footwork’ ndio balaa, kubwa kabisa unao mwili mzuri wa kuwa namba nine, na unajua kutumia nguvu zako na bila kusahau uwezo ulionao wa kucheza mipira ya kichwa.”

“Lakini bado hujafika kokote katika ndoto zako na hata matarajio yetu kwako, una mengi mno ya kuboresha kiwango chako na kuendelea kujifunza zaidi, hivi vigoli ulivyofunga visikupandishe mabega na vitumie kama mwanzo wa safari yako ndefu kwenye soka”.

“Tunza mwili wako kwa nidhamu ya kifutboli, usiuchoshe pale unapohitajika kupumzishwa na katika hili hukatazwi kula ujana wako, ‘but make sure’ unafanya kwa kiasi bila kuathiri kiwango chako”.

“Penda kufanya ‘extra training’ ukiacha yale ya timu, uliza Wachezaji wakubwa hapo nini uboreshe, ongea nao sana pamoja na Makocha wako, kisha nenda kamsome King Pele kwenye kitabu chake ‘My life and beautiful game’ ana mengi ya kukufunza hususan kwenye rika lako.

“Mwisho nakuomba sana achana na Washauri Wapuuzi wanaokujaza kwa sifa za kijinga, nimeona ‘somewhere’ eti wanakwambia wewe ni bora kuliko Fiston Mayele, wanakuongopea na hawana nia njema na wewe, Mayele ni kitabu kamili cha jinsi Mshambuliaji anatakiwa awe, jifunze sana kwake na siku moja utavaa viatu vyake”.

“Washauri wa aina hiyo na wale watakaotaka ufanye nao kama Meneja wasikilize ila ingiza pamba masikioni, wengi washapotea kabla yako kwa hawa wajuaji wasio wema”.

“Fursa uliyopata Yanga SC ni kubwa mno, usikubali kuipoteza kirahisi Kwa kusikiliza ngonjera za Maabunuwasi, wekeza akili, muda, maarifa, nguvu na jasho lako hapo ulipo, huku ukisubiria wakti sahihi wa kutoboa zaidi”.

Ahh leo acha niishie hapa, mengine mengi tutaongea baada ya hizi holidays.

Shukran Clement ๐Ÿ™๐Ÿป


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...