BENKI ya Exim Tanzania imeendelea kugawa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu na simu janja (smartphones) kwa washindi wa kampeni yake “Chanja Kijanja, Kimasta Zaidi’’ inayolenga kuhamasisha wateja wa benki ya Exim kutumia kadi zao za Mastercard katika manunuzi ya mtandaoni au kufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS) katika maduka mbalimbali na maeneo mengine nchini.
Kampeni hiyo iliyozinduliwa mapema mwezi Novemba inatoa
fursa kwa wateja wa benki hiyo wanaotumia kadi zao za Exim Mastercard
kufanya miamala, kuwa kwenye nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali
ikiwemo fedha taslimu, Simu janja (Smart Phones) na safari zilizolipiwa
gharama zote kwenda mapumziko katika mataifa ya Dubai, Uturuki na Afrika
Kusini wao pamoja na wenza wao.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya
kukabidhi zawadi hizo kwa washindi hao ikiwemo zawadi ya simu janja
aina ya Iphone 14 Pro kwa mshindi wa mwezi ambae ni Bw Emanuel Lutambi
mkazi wa mkoa wa Iringa, Afisa Idara ya Huduma Mbadala Kupitia Mifumo ya
Kidigitali wa Benki ya Exim Bw Gregory Malembeka alisema hadi kufikia
sasa zaidi ya washindi 100 wameshajishindia zawadi ya fedha kiasi cha
Tsh 100,000 kila mmoja kupitia droo “bahati nasibu” na mitandao.
“Inafahamika
kwamba kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka kinahusisha manunuzi
zaidi kutokana na sherehe na sikukuu ya Christmas. Wito wetu kwa wateja
wetu ni wao kufanya manunuzi kwa kutumia Exim Mastercard iwe mtandaoni
au kwenye mashine za malipo (POS) ili waweze kujiweka kwenye nafasi ya
kushinda kwa kuwa zawadi bado ni nyingi.’’
“Ifahamike kwamba
unapochanja au kulipia bidhaa au huduma basi unajiweka kwenye nafasi ya
kuingia kwenye droo ya kushinda safari zilizolipiwa kila kitu kikamilifu
kwa siku tano kwenda Dubai, Uturuki au Afrika Kusini pamoja na mpendwa
wako. Pia unaweza kuwa mshindi wa iPhone 14 pro inayotoka kila mwezi au
pesa taslimu100,000 inayotoka kila wiki….ujanja ni kuchanja tu na Exim
Mastercard’’ Alisema.
Meneja wa Benki ya Exim tawi la Mkoa wa Iringa Bw Michael Richard (wa pili kushoto) sambamba na maofisa wengine wa benki hiyo Bi. Aziza Msangi (kushoto) na Bw. Emanuel Bayo (Kulia) wakikabidhi zawadi ya simu janja aina ya Iphone 14 Pro kwa Bw Emanuel Lutambi mkazi wa mkoa huo baada ya kuibuka mshindi wa droo ya mwezi ya kampeni ya “Chanja Kijanja, Kimasta Zaidi’’ inayolenga kuhamasisha wateja wa benki hiyo kutumia kadi zao za Mastercard katika manunuzi ya mtandaoni au kufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...