Afisa Utumishi Mwanamizi wa Manispaa ya Temeke Grace Mtisho akikata utepe kuashiria uzinduzi wa makubaliano ya Kituo Kimoja cha Biashara (One Stop Business Center) kati ya Danube Home na Furniture Centre uliofanyika Leo jijini Dar es Salaam. Afisa Utumishi Mwanamizi wa Manispaa ya Temeke Grace Mtisho alimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Furniture Centre, Prasad Kumar na wa pili kulia ni Meneja wa kampuni ya Kuuza Samani ya Danube Home, Mahfooz Gafoor
DANUBE HOME, kampuni kutoka Dubai, wameanza biashara rasmi Tanzania leo hii kwa kufungua duka lao jipya wakishirikiana na Furniture Centre.
Danube Home ni wauzaji wa samani (furniture) na wameamua kufungua duka hili kwa kushirikiana na Furniture Centre kwa kutambua kuwa Furniture Centre ni wauzaji wakongwe wa samani nchini (Furniture) kwa takribani miaka 65.
Afisa Utumishi Mwanamizi wa Manispaa ya Temeke Grace Mtisho akizungumza kuhusu namna Serikali inavyotambua mchango wawa Kampuni hiyo yenye zaidi ya Miaka 65 ya kufanya kazi hapa nchini ambapo maduka yao yapo kwenye Mikoa kama Dodoma, Mwanza, Arusha na Dar es Salaam ambapo wameweza kuajili watu zaidi ya 300 ambao wote hawa ni watanzania kabisa ikiwemo kuwapangia Nyumba ili wasikae mbali na ofisi hivyo hii Kampuni ni sehemu ya Taifa hivyo wananchi wa kawaida waje kununua bidhaa zao kwenye maduka ya Danube wakati wa uzinduzi wa makubaliano ya Kituo Kimoja cha Biashara (One Stop Business Center) kati ya Danube Home na Furniture Centre yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Afisa Utumishi Mwanamizi wa Manispaa ya Temeke Grace Mtisho alimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya
Mkurugenzi Mkuu wa Furniture Centre, Prasad Kumar akizungumzia historia ya Kampuni hiyo iliyoanzishwa mwaka 1956 hapa nchini pamoja na walivyifanya maamuzi kuweka makubaliono kati ya Kampuni Furniture Centre pamoja na Danube Home ya kuweka Kituo kimoja cha kufanya Biashara ya Samani za ndani ambacho ni Kituo Kimoja cha Biashara (One Stop Business Center) kwenye uzinduzi uliofanyika Leo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa kampuni ya Kuuza Samani ya Danube Home, Mahfooz Gafoor akizungumza namna walivyijipanga kushirikia na Kampuni ya Furniture Centre ili kuweza kutoa Huduma Bora wa wateja wao wakati wa uzinduzi wa makubaliano ya Kituo Kimoja cha Biashara (One Stop Business Center) kati ya Danube Home na Furniture Centre yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Afisa Mwajili mkuu wa Manispaa ya Temeke Grace Mtisho(wa Tatu kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja Uendeshaji wa Furniture Centre, Faiza Adam(wa kwanza kushoto) mara baada ya kufanya uzinduzi wa makubaliano ya Kituo Kimoja cha Biashara (One Stop Business Center) kati ya Danube Home na Furniture Centre yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Furniture Centre, Prasad Kumar na wa pili kulia ni Meneja wa kampuni ya Kuuza Samani ya Danube Home, Mahfooz Gafoor
Meneja Uendeshaji wa Furniture Centre, Faiza Adam akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Afisa Mwajili mkuu wa Manispaa ya Temeke Grace Mtisho kwa kushiriki katika uzinduzi wa makubaliano ya Kituo Kimoja cha Biashara (One Stop Business Center) kati ya Danube Home na Furniture Centre yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...