Na Jane Edward, Arusha
Waziri wa maliasili na utalii Dr Pindi Chana amewataka Watanzania na wadau wa sekta ya utalii kuendeleza sekta hiyo katika nyanja mbalimbali ili kurithisha vizazi vya sasa na baadae katika masuala ya urithi wa Dunia.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha katika Mkutano wa masuala ya urithi wa Dunia uliozikutanisha nchi mbalimbali kwa lengo la kutambua maeneo ya urithi wa dunia ikiwemo hifadhi ya Ngorongoro, Serengeti,Mlima Kilimanjaro pamoja na michoro inayopatikana Kondoa.
Chana amesema Mkutano huo umeunganisha nchi kadhaa ikiwa na lengo la kuendeleza kutoa elimu ya namna ya kuelewa masuala ya urithi wa Dunia.
Amesema kuwa katika sekta ya Utalii Kuna weza kuweka mtaala maalum katika sekta ya elimu wa kuweza kufundisha na kuyalinda maeneo ya urithi wa dunia na kutambua namna ya kuweka sehemu kubwa ya kivutio na kuongeza kipato.
"Sasa hivi utalii unachangia asilimia 17 ya pato la Taifa,ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja takribani Ml 1.5 ambapo mpaka sasa hakuna eneo maalumu lililoweza kutafsiriwa kama eneo la urithi wa Dunia"Alisema Chana
Aidha Waziri chana amesema katika kuadhimisha miaka hamsini ya mkataba wa Kimataifa wa urithi wa Dunia na kuiomba UNESCO kuifanya Tanzania kuwa sehemu ya kufanya mikutano hiyo kila wakati.
Kwa upande wake Mohamed Juma Mohamed Mkuu wa dawati la Afrika katika kitengo cha urithi wa Dunia amesema kuwa wanasherehekea miaka hamsini na kuangalia masuala ya elimu katika miaka hamsini ijayo.
Amesema kuwa katika sekta ya urithi wa dunia bado changamoto ni kutokuwepo kwa wataalamu wakike na kwamba vyuo viangalie nafasi ya kuanza kufundisha masuala hayo ili kuwa na wataalamu wengi wabobezi.
Waziri wa maliasili na utalii Dr Pindi Chana akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela katika mkutano wa Masuala ya urithi wa dunia jijini Arusha.
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...