Na Mwandishi Wetu-KIGALI,RWANDA
MKURUGENZI
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA)
Mhandisi Modestus Lumato,ameiwakilisha Mamlaka hiyo katika Mkutano wa
Jumuiya ya Wadhibiti wa Nishati Afrika Mashariki (EREA), kujadili
masuala mbalimbali ya ushirikiano katika udhibiti wa sekta ya Nishati .
Mkutano huo umefanyika leo Desemba 13,2022 jijini Kigali nchini Rwanda.
Mkutano
huo umehudhuriwa na wanachama wake ambao ni taasisi za udhibiti kutoka
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni AREEN ya Burundi, EPRA ya
Kenya, ERA ya Uganda, PURA ya Tanzania, ZURA ya Zanzibar, ARE ya DRC,
RURA ya Rwanda na EWURA ya Tanzania.
Kikao kazi hicho
kitafuatiwa na Mkutano wa Bodi Huru ya Kiudhibiti (IRB - Independent
Regulatory Board) inayosimamia Muungano wa Taasisi za Nishati za Afrika
Mashariki (East African Power Pool ) kuanzia tarehe 15 Desemba 2022
jijini Kigali ambapo Djibouti , Ethiopia na Misri pia zitashiriki.
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato,(mbele kushoto), akishiriki Mkutano wa Jumuiya ya Wadhibiti wa Nishati Afrika Mashariki (EREA) unaojadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika udhibiti wa sekta ya Nishati uliofanyika leo Desemba 13,2022 Mjini Kigali, Rwanda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...