Rais Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education - GPE) akingoza Vikao vya Bodi ya Taasisi hiyo vinavyofanyika Jijini Paris, nchini Ufaransa kuanzia tarehe 5 - 7 Disemba, 2022.
Vikao hivyo ni vya kwanza vya ana kwa ana tangu dunia ilivyokumbwa na ugonjwa wa COVID-19 mwishoni mwa mwaka 2019. Katika vikao hivyo, Taasisi ya GPE inapitia na kuazimia masuala mbalimbali yatakayolenga kuboresha mifumo ya elimu katika nchi zinazoendelea ikiwemo kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata elimu, wakiwemo watoto wa kike, na matumizi ya teknolojia katika utoaji wa elimu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...