Na.Khadija Seif ,Michuzi TV

MSANII wa vichekesho  Lucas Mhuvile maarufu Joti amefunguka na kuweka wazi namna alivyojipanga katika kuhakikisha anaipambania tuzo ya Mchekeshaji bora katika tuzo za Filamu  zinazotarajiwa kufanyika Jijini Arusha Disemba 17,2022 na kwamba atashinda kwa kishindo.

Akizungumza na Michuzi tv Joti ameeleza namna alivyo na kitete pamoja na hofu kwenye kinyang'anyiro hicho kwa msimu wa pili huku akifafanua zaidi hana shaka na ubora wa kazi zake akiwaomba sana watanzania na wapenzi wa kazi zake kumpigia kura kwenye vipengele viwili  alivyofanikiwa kuingia katika kinyang'anyiro ikiwemo kipengele cha  filamu bora ya ucheshi na Mchekeshaji bora wa mwaka kipengele hicho kikiwaniwa na wasanii mbalimbali akiwemo  Mkojani,Gladness Kifaluka, Tabu Mtingita pamoja na brother K.

Aidha filamu bora ya vichekesho ambazo zimefanikiwa kuingia ni "usipite jeshini" ya joti,Mama mkwe ya tabu Mtingita pamoja na msanii Brother K katika vichekesho vya futuhi,Gladness kifaluka wa filamu ya kitimtim na Mkojani akiingia na filamu ya Ugaigai.

Hata hivyo Joti ameeleza namna kuwepo kwa tuzo hizo zimesaidia sana tasnia ya filamu kukuwa na kuimarika kutokana na uwepo wa ushindani pamoja na Serikali kutambua mchango wa tasni ya filamu.

"Kwa mara ya pili nashiriki tuzo hizo kwa mwaka jana zilifanyika Mkoani Mbeya na nikifanikiwa kushinda tuzo mbili ikiwemo Mchekeshaji bora wa mwaka 2021 pamoja na  filamu bora ya vichekesho.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...