Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Simu ya TECNO imesema kwamba kwa mara ya kwanza katika historia wameshuhudia msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka ukiwa na burudani kubwa ya mchezo wa mpira wa miguu duniani (Fainali za Komba la Dunia) ambazo zinaendelea huko Qatar.

Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo iliyotolewa leo Desemba 14,2022 imeelezwa kuwq fainali hizo ambazo zilianza kutimua vumbi Novemba 20 mwaka huu zinatarajiwa kukamilika Disemba 18 mwaka huu hivyo kufanya burudani hiyo kukutana na msimu wa sikukuu ya Chrismas na Mwaka Mpya.
"Mambo mengi yakufurahisha wateja yanaendelea kufanywa na Makampuni mengi ambapo katika upande wa simu Kampuni ya TECNO inaendelea kuupiga mwingi na kampeni ya ‘Sambaza furaha’. Tukiwa tumebakiwa na siku chache kuhitimisha mchuano huu wa kombe la dunia TECNO inakuhabarisha campaign ya ‘Sambaza furaha’ bado inaendelea.

" IPost picha ya umpendae ikiambatana na ujumbe mzuri #Sambazafuraha @tecnomobiletanzania au unaweza jizawadia wewe mwenyewe kwa kupost picha yako ikiambatana na ujumbe mzuri kisha tag na kuhashtag kama inavyojieleza hapo juu."

Kampuni ya TECNO imesema zinatolewa kila siku kwa mshiriki ambaye ujumbe wake umeonekana kuvutia wengi na kupata likes na comments nyingi, kila siku hadi Kuelekea Kombe la Dunia simu aina ya TECNO Camon 19 na Spark 9 zitaendela kutolewa kwa washiriki wanaokidhi vigezo."Tembelea @tecnomobiletanzania au piga nambari 0744545254, 0678035208."


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...