Kiwanda cha kutengeneza na kuunganisha magari nchini Tanzania GF cha Vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwan kimeibuka mshindi wa kwanza kwa makampuni makubwa nchini wakati wa utoaji wa tuzo za Ubora wa Kitaifa wa makampuni bora kwa Mwaka 2022\2023 zilizoandaliwa na shirika la viwango nchini TBS.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Kiwanda cha hicho, Ezra
Mereng alisema wanaipokea tuzo hiyop kwa furaha kutokana na kushiriki
kwa mara ya kwanza na kuibuka kuwa washindi wa jumla katika kipengele
cha makampuni makubwa,
Pia alisema tuzo hiyo inawahasisha kuendelea
kufanya kazi kwa bidi Zaidi ikiwezekana mwakani washinde tuzo za
kimataifa za ubora wa bidhaa na itakayoweza kuzalisha magari na kuingia
katika soko la ushindani kimataifa.
Pia aliwashukuru wafanyakazi wenzake wakiongozwa na timu mzima ya wataalamu katika kutengeneza magari vitengo tofauti .
Nae
mkurugenzi wa shirika la viwango nchini (TBS) Dr. Athuman Ngenya
aliwataka GF kutoridhika na ushindi huo wa jumla nchini na wahakikishe
wanashiriki mashindano ya nchi ya SADC katika ubora na viwango kwa
makampuni ya jumuia hiyo kuibukja mshindi anapata tiketi ya moja kwa
moja ya kushiriki mashindano ya Uboroa na viwango ya jumuia ya SADC na
atakuwa anaiwakilisha Tanzania na wao kama TBS watashirikiana na GF
kuhakikisha wanapeperusha vyema benderaya Tanzania.
Kwa kumalizia
mkurugenzi Mtendaji wa GF Vehicles Assemblers (GFA) Imrani Karmal
anawapongeza wafanyakazi wake kwa umoja wao ndio chachu ya mafanikio ya
wao kukidhi Ubora katika uzalishaji wa magari bila wao wasingweweza
kufanikiwa katika ushindi huo,Pia ameupokea ushauri wa mkurugenzi wa TBS
wa lkumtaka kushiriki mashindano ya SADC ya ubora na viwango .
Akimalizia
Karmali alisema kutokana na mazingira rafiki ya uwekezaji na mahusiano
mazuri na serikali Kiwanda hicho kipo katika hatua ya pili ya upanuzi
ili kuweza kuzalisha magari aina zoote makubwa(truks) na madogo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt.Athuman Ngenya(kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GF Vehicle Assemblers Limited,Imran Karmali tuzo ya Ubora wa Kitaifa wa Kampuni bora ya Mwaka 2022\2023 kwa makampuni makubwa wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo hiyo iliyoandaliwa na TBS. jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mkuu wa GF Vehicle Assemblers, Bw. Ezra Mereng
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt.Athuman Ngenya(kushoto) akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GF Vehicle Assemblers Limited,Imran Karmali wakati wa kupokea tuzo ya Ubora wa Kitaifa wa Kampuni bora ya Mwaka 2022\2023 kwa makampuni iliyoandaliwa na TBS jijini Dar es Salaam . Kulia ni Meneja Mkuu wa GF Vehicle Assemblers, Bw. Ezra Mereng
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...