Njombe
Ligi ya Swalle Cup 2022 Imemalizika katika Jimbo la Lupembe Kwa kuzikitanisha timu ya Igongolo iliyoibuka kidedea na kukabidhiwa kombe pamoja na Ng'ombe mwenye Thamani ya Tsh Mil.1
Mchezo wa fainali umezikutanisha timu ya Igongolo pamoja na timu ya kata ya Mfriga ambapo timu kutoka kata ya Igongolo Imeibuka Mshindi katika fainali hizo kupata magoali 3 - 1 yaliyopatikana katika mikwaju ya Penati mara baada ya kutoshana nguvu katika dakika 90 za mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa kijiji cha Wanginyi.
Mbunge wa jimbo la Lupembe mkoani Njombe Edwirn Swalle pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe wamekabidhi kombe pamoja na Ng'ombe mwenye thamani ya T'sh Mil.1 kwa timu ya Igongolo kwa kuwa bingwa wa michuano hiyo huku akiahidi maboresho makubwa kila mwaka kwenye ligi hiyo.
"Niliwaambia mwaka jana haya mashindano ya Swalle Cup kila mwaka yatakuwa yanapanda thamani,na kuanzia mwakani tutakuwa na Swalle Cup Maalumu Kwa shule za sekondari zote za Jimbo la Lupembe"Edwirn Swalle Mbunge wa Lupembe
Aidha Swalle ameahidi kupeleka baadhi ya vijana wa jimbo hilo kusomea kozi za uamuzi Ili kuendelea kuboresha ligi mbali mbali zinazoendelea katika Jimbo la Lupembe"Kuanzia mwakani nitapeleka marefalii kusomea urefa"alisema Swalle
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...