-Ni lilofanyika Msitu wa Vikindu, Mkuranga asema Matamasha kama haya yanatakiwa kufanyika Tanzania nzima

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amefurahishwa na Tamasha la Bata Msituni ambalo liliandaliwa na Chinobychino Travel kwa kushikiriana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambapo amesema kuwa matamasha kama hayo yanatakiwa kufanyika Tanzania nzima ili watu wafurahi.

Mhe. Mchengerwa alisema hayo wakati akizindua Tamasha hilo lililofanyika Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia Pugukazimzumbwi Safu ya Vikindu uliochini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS). Alisema Watanzania wanafanya kazi sana hivyo baada ya majukumu yao ni muhimu kupumzika na hivyo matamasha kama hayo ni muhimu sana.

Aidha, Mhe. Mchengerwa aliwapongeza waandaaji kwa kuwa na ubunifu huo mkubwa na kuwasihi waendelee kuandaa matamasha hayo zaidi huku wakiwahusisha mamlaka husika.

Mgeni Rasmi Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi ambapo alipongeza ubunifu huo na kusisitiza kuwa matamasha kama haya yanatakiwa kufanyika Tanzania Nzima, alizungumza hayo wakati wa Tamasha kubwa la Bata Msituni Lililofanyika katika Msitu wa Vikindu Safu ya  Pugu Kazimzumbwi
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija Nassir akitoa salamu za shukurani kwa muitikio Mkubwa wa watu waliofika katika Tamasha la Bata Msituni lililofanyika katika Msitu wa Vikindu safu ya  Pugu Kazimzumbwi  uliochini ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS)


Malkia wa Mipasho Bi. Khadija Kopa akitoa burudani ya nguvu huku watu wakifurahia wakati wa Tamasha kubwa la Bata Msituni ambalo lilifanyika katika msitu wa Vikindu Safu ya Pugu Kazimzumbwi  ambao Msitu huo upo chini ya Wakala wa Misitu Tanzania TFS


Wanamwita Chui, Rayvan hapa akiwa anakiwasha wakati wa Tamasha la Bata Msituni ndani ya Msitu wa Pugu Kazimzumbwi Safu ya Vikindu Mkuranga , Msitu huo upo chini ya wakala wa Misitu Tanzania TFS

Ukisikia piga kigoma mpaka unaamka ni hiki sasa Mgeni Rasmi Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa, hapa akaona hapana ikabidi aungane na wanabata msituni kufurahia Tamasha kubwa la Bata Msituni huku Kigoma kikiendelea. (Picha na Fredy Njeje Mdau wa Utalii)
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...