Njombe

Vijana wa halmashauri ya mji wa Njombe wameshauriwa kujiunga kwenye vikundi na kuchangamkia mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa na halmashauri yao ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe Erasto Mpete ambaye ni diwani wa kata ya Utalingolo katika fainali za michuano ya Mpete Diwani Cup Iliyofanyika katika uwanja wa Nole mjini humo.

“Halmashauri yetu ya mji ina mikopo ya vikundi lakini changamoto inayoonekana vikundi vya vijana hatuchangamkii hiyo fursa,kwa hiyo kupitia haya mashindano ninahamasisha vijana muweze kujiunga kwenye vikundi ili muweze kupata fursa hii ya mikopo isiyokuwa na riba”amesema Erasto Mpete

Mgeni rasmi katika michuano hiyo Mh,Basilius Namkambe Nyangachi ambaye ni mkuu wa Mashtaka mkoa wa Iringa awali akifungua fainali za michuano hiyo ametoa wito kwa vijana kujituma na kuweka juhudi kwenye michezo kwa kuwa vipaji ni ajira huku pia akitoa wito kwa wananchi kusomesha watoto ili waweze kuwasaidia baadaye.

Baadhi ya vijana walioshiriki kwenye michuano hiyo wamemshukuru diwani kwa kuanzisha ligi hiyo ambayo imewakutanisha vijana mbali mbali na kujifunza mambo mengi huku wakiimarisha afya zao.

Mpete Diwani Cup 2022 imetamatika mjini Njombe ambapo timu Mfereke FC imeibuka na ushindi wa goli 1 kwa 0 dhidi ya Nole FC katika uwanja wa Nolen a kujinyakulia kitita cha fedha T’sh 500,000 pamoja na kombe lenye thamani ya T’sh 200,000 huku mshindi wa pili Nole FC akijinyakulia kititia cha T’sh 300,000 na Mshindi wa Tatu Ihalula akijipatia shilingi laki 200,000 huku zawadi hizo pia zikiambatana na zawadi nyingine ndogo ndogo.

Aidha diwani wa kata hiyo Erasto Mpete ameahidi kuongeza thamani Zaidi ya michuano katika msimu ujao huku akiongeza ligi ya wanawake kwa kuanza na wanafunzi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...