Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Deogratius Ndejembi akizungumza ma washiriki wa 13 la la wataalamu wa ununuzi na ugavi 
Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya wataalam wa ununuzi na ugavi PSPTB Godfrey Mbanyi katika mkutano huo Jijini Arusha
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la 13 la mwaka la wataalamu wa ununuzi na ugavi lenye kauli mbiu ya Ununuzi wa kimkakati ;fursa na changamoto katika kutekeleza ukuaji endelevu wa uchumi na maendeleo ya jamii,katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICCC Jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la 13 la mwaka la wataalamu wa ununuzi na ugavi lenye kauli mbiu ya Ununuzi wa kimkakati ;fursa na changamoto katika kutekeleza ukuaji endelevu wa uchumi na maendeleo ya jamii.


Na.Vero Ignatus,Arusha.
 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Deogratius Ndejembi amesema Ili kuweza kuleta tija kwenye miradi ya kimkakati Serikali lazima ijielekeze kufanya ununuzi wa kimkakati kwa kuzingatia ukubwa wa ununuzi wa serikali na sekta za umma kwa ujumla.

Akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la 13 la mwaka la wataalamu wa ununuzi na ugavi lenye kauli mbiu ya Ununuzi wa kimkakati ;fursa na changamoto katika kutekeleza ukuaji endelevu wa uchumi na maendeleo ya jamii,...amesema ni imani yake kuwa kupitia majadiliano na mada mbalimbali zitakazowasilishwa zitawajengea uwezo na ufanisi katika kutekeleza miradi hiyo.

Aidha amewataka wataalam haku kuchukuwa hatua kwa kuzingatia sheria,taratibu na kanuni ili kuhakikisha wataalam hao wanafanya kazi za ununuzi na ugavi kwa weledi na ujuzi kwa wataalam hao wanamchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi.

Ameongeza kwa kuipongeza bodi hiyo kwa kuandaa mtaala unaozingatia ujuzi na umahiri wa kitaaluma na mahitaji ya soko kama ambavyo bodi hiyo ilivyojikita kuzalisha wataalam wenye uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa na kuhakikisha taaluma ya ununuzi na ugavi inaleta mapinduzi chanya katika malengo ya serikali na sekta binafsi.

Mhe.Ndejembi amewaelekeza waajiri wote nchini kuhakikisha wanaweka watu wenye sifa ya taaluma ya ununuzi na ugavi kusimamia idara za ununuzi na ugavi sambamba na kupeleka wasiokuwa na sifa hizo shule kuwaendeleza pamoja na waajiri kuzingatia mahitaji ya waraka namba 3 ya mwaka 2015 ya muundo wa utumishi ili kuhakikisha watumishi wote wanasifa stahiki za kitaaluma.

Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya wataalam wa ununuzi na ugavi PSPTB Godfrey Mbanyi katika mkutano huo amesema kuwa bodi itaendelea kuchukuwa hatua madhubuti ya kusimamia weledi na maadili ya wataalamu wa ununuzi na ugavi waliosajiliwa ili kuweza kukidhi usimamizi wa sheria.

Aidha alisema kuwa  kongamano hilo litapokea mrejesho wa maazimio ya utekelezaji wa kongamano la 12 ili kubainisha changamoto za utekelezaji katika ununuzi wa kimkakati kusudi ziweze kujadiliwa.

Vilevile amesema mafunzo na usajili unaofanyika unasaidia bodi kupata wataalam wenye sifa stahiki na weledi kwenye soko la ajira na kurahisisha utekelezaji wa sheria katika uratibu na udhibiti wa maadili na mienendo ya wataalam wa ununuzi na ugavi.

Awali Mwenyekiti wa Bodi hiyo Jacob Kibona ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kudumisha utawala bora ambao unaweka mazingira wezeshi katika utekelezaji wa sheria ya ununuzi wa umma na kuhakikisha taaluma,kanuni na taratibu zinazingatiwa kwa uhuru na kwa ufanishi bila kuingiliwa.

"Pamekuwepo na dhana kwamba panapotokea kasoro basi afisa ugavi pekee ndiye anayehusika,lakini panapokuwa na mafanikio mazuri na taasisi husika ikapongezwa,afisa ugavi na ununuzi huwa hatokei."alisema ....

Aliongeza kuwa bodi inayo wajibu wa kuwaadhibu wataalam wake pale inapothibitika kuwepo kwa itendaji mbovu,na kuahidi kuwa bodi haitasita kuchukuwa hatua za kknidhamu baada ya kujiridhisha kwamba aliyetenda kosa ni afisa manunuzi na siyo mtu mwingine.

Sambamba na hayo ameongeza kuwa katika kusimamia taaluma ya ununuzi na ugavi,bodi itaendelea kutoa mafunzo endelevu kwa wataalamu wake pamoja na wadau mbalimbali kwenye mnyororo wa ununuzi na ugavi ambapo pia bodi hiyo inakusudia kuleta mabadiliko yenye tija kwa wataalamu wa ununuzi na ugavi ,idara atamizi na kuboresha misingi ya taaluma itakayoweza kukabiliana na mabadiliko yatokanayo na maendeleo ya taaljma yenye kukidhi haja ya soko la ajira katika uchimi shindani wa viwanda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...