Na Mwandishi Wet, Michuzi TV

MKURUGENZI wa Taasisi ya Viwango Zanzibar(ZBS) Yusuph Nassor amechukua fomu ya kuwania Nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Januari 29 Mwaka 2023 .

Kamati ya Uchaguzi wa Simba ilifungua mlango wa kuchukua fomu Desemba 5 kwa wagombea wenye nia ya kuwania nafasi mbalimbali ikiwemo ya Uenyekiti ambayo kwa Sasa ipo chini ya Murtaza Magungu aliyeuchaguliwa kwenye uchaguzi mdogo baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Swedy Mkwabi kujiuzuru.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo Nassor ambaye aliyewahi kuwa Mkuu wa Kitengo Cha Fedha ,Utawala na Uendeshaji cha Klabu hiyo amesema ameamua kutumia nafasi yake hiyo ya kikatiba Ili kuingoza Klabu hiyo kongwe baada ya kuona ana kila sababu ya kuhakikisha ana iletea maendeleo.

"Ninaifahamu vizuri Simba kwani mbali ya kuwa kwanza nina mapenzi nayo kwa kipindi kirefu, pia nimefanya nayo kazi vizuri hadi wakati huu nilipoamua kuchukua fomu hii, malengo yangu ni kuiongoza na kuifikisha mbali zaidi kimafanikio" amesema Nassor

Amesema kupitia nafasi mbalimbali za uongozi anazozitumikia na alizowahi kuzitumikia kwa nyakati mbalimbali atahakikisha anaiongoza klabu hiyo na kuipa mafanikio makubwa katika mchezo wa mpira wa miguu ndani na nje ya nchi.

"Sote tunatambua kuwa Simba imepata mafanikio makubwa , malengo yangu ni kuifikisha mbali zaidi kwa kushirikiana na viongozi wenzangu na hiyo ndiyo hasa sababu kuu iliyonifanya nijitokeze kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti" ameongeza Nassor

Simba wanafanya uchaguzi huo baada ya viongozi waliopo madaraka kuongoza kwa miaka minne kwa mujibu wa katiba ambapo nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti na wajumbe wanne pekee.

Kwa mujibu wa katiba yao, mwenyekiti atakayechaguliwa ana nafasi ya kuteua wajumbe wawili ambao wataingia kwenye Bodi ya Wakurugenzi wakitimiza idadi ya wajumbe saba kutoka upande wa klabu kuingia katika bodi hiyo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...