MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salam, Khadija Ally, amesema hataki machawa na badala yake anataka viongozi na wanachama wa jumuiya hiyo kuchapa kazi.

Akizungumza leo Desemba 14, 2022 katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam Khadija amesema yeye sio Mwenyekiti wa Chawa ,hivyo anachotaka kuona viongozi na wanachama wa jumuiya hiyo wanafanya kazi kuanzia ngazi ya Kata, kuangalia malenzi ya Watoto, maadili na elimu katika shule zinazomilikiwa na jumuiya hiyo.

“Tufanye kazi zionekane, jamii ifaidike, tuwe viongozi wenye maadili, viongozi tunapaswa kuwa mfano wa kuigwa, hatuwezi kuwa viongozi ambao hatuna maadili,"amesema Mwenyekiti huyo

Ametumia nafasi hiyo kueleza anaandaa mafunzo maalum ya uongozi yenye lengo la kukumbushana misingi ya jumuiya, maadili ya uongozi na malezi.

“Hatuwezi kuwa na kiongozi asiye na maadili, tuwe na uongozi shirikishi sio uongozi wa kimungu, utakachosema ndio hicho hicho .Hutaki ushauri, hutaki kusikia lolote kwa mtu yoyote, hapana! uongozi lazima uwe shirikisho.”

Aidha, katika kikao hicho pia umefanyika uchaguzi mdogo wa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya jumuiya hiyo.Walioshinda nafasi ya Baraza la Mkoa na Kamati ya utekelezaji Wazazi Mkoa ni Omar Ngurangwa, Muhammad Abdulghafur na Busoro Pazi.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...