-wasanii watembelea vivutio vya utalii Arusha
Na.Khadija Seif, Michuzi TV
WASANII wa Filamu nchini Leo Disemba 16,2022 wametembelea Vivutio vya utalii vilivyopo Moshi Mkoa wa Kilimanjaro huku wakiomba vibali kuwa na bei rafiki ili wazalishe kazi nyingi ndani ya Vivutio vya utalii.
Akizungumza na Michuzi TV Mkongwe wa Filamu hapa nchini, Abdulaziz Babu amesema ni wakati wa wasanii kutumia vivutio hivyo kumalizia kazi aliyoianza Rais Samia Suluhu katika Filamu ya Royal Tour.
"Mama amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watalii wanafika nchini Tanzania kuona vivutio vilivyopo hivyo wasanii ni kazi kwao kuendeleza juhudi hizo kupitia tamthilia na Filamu wanazozalisha walau kuwepo kwa vipande vinavyoonyesha utalii wetu ikiwemo Misitu,uoto wa asili pamoja na mandhari ya maeneo ya misituni."
Hata hivyo babu amewaomba wasimamizi wa vivutio hivyo kuweka bei rafiki kwa vibali vya wasanii kuyatumia maeneo ya hifadhi ya utalii ili kuwepo utayari kwa watayarishaji wengi kufika katika hifadhi mbalimbali nchini katika kutangaza vivutio vya utalii.
Nae Mkongwe wa tasnia ya Filamu Ahmed Olotu a.k.a Mzee chilo amesema kupitia Bodi ya Filamu imempa fursa kama Msanii kutembelea kando kando ya Hifadhi ya Mlimani Kilimanjaro.
"Tunaona umuhimu wa kuwa na tuzo hizi sio tu ushindani bali wasanii kupata fursa ya kujifunza ,kuwa na uzalendo na kuongeza ujuzi kwa kupata maeneo mengi (Location) ya kutengeneza kazi zao hivyo kiukweli tumepata hamasa kubwa sasa hususani kwa watayarishaji kutengeneza kazi ndani ya vivutio vya utalii. "
Kwa upande wake Neema walele a.k.a Brenda ametoa ahadi ya kuwa Mtayarishaji wa kwanza kufika Hifadhi ya pembezoni mwa Mlimani Kilimanjaro kutengeneza Filamu yake mwakani.
"Tumekuwa na dhana ya kuamini kuwa kuna ugumu katika kufika katika vivutio vya utalii lakini niwatoe hofu wadau wa Filamu kutengeneza kazi zao katika vivutio vya utalii na kufata masharti n kulipia vibali haiwezekani wageni waje nyumbani kwako watumie vitu vyako ambavyo wewe mwenye huvipi kipaumbele kuvitumi sasa ni wakati wetu wasanii kutumia vivutio vyetu kwenye Filamu zetu ambazo hata zikifika kwenye soko la Kimataifa tutakuwa tunaendelea kutangaza upekee wetu uliopo nchini Tanzania. "
Aidha wasani hao wametembelea vivutio mbalimbali ikiwemo pembezoni mwa Mlima Kilimanjaro,Maporomoko ya Maji yaliyopo Materuni pamoja Msitu wa Rau uliopo Moshi Mkoan Kilimanjaro.
Wasanii mbalimbali waliotembelea Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro akiwemo Mkongwe wa tasnia ya Filamu Mama Thecla Mjata,Big Matovolwa, Mzee chilo pamoja na Msanii chipukizi Regina
Mkongwe wa tasnia ya Filamu nchini Ahmed Olottu a.k.a Mzee chilo akiwa na wasanii wenzake wakisoma baadhi ya maelezo yaliyopo katika hifadhi ya Mlima Kilimanjaro Moshi Mkoani Kilimanjaro wakati wa kutembelea vivutio mbalimbali
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...