Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeendelea kugawa zawadi kwa washindi mbalimbali wa kampeni yake ya ‘Vuna zaidi na NBC Shambani’ msimu wa pili inayoendeshwa katika mikoa ya Mtwara na Lindi zikiwemo baiskeli, pikipiki, guta, pampu za kupulizia dawa, huku serikali ikibainisha kuwa zawadi hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuchochoea kasi ya uzalishaji wa mazao ya korosho na mazao mengine katika mikoa hiyo.

Hafla fupi ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi wa droo ya pili ya kampeni hiyo ilifanyika wilayani Masasi, Mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki ikipambwa na uwepo wa wakuu wa wilaya ya Masadi Bi Bi Claudia Kitta, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Bi Bi. Mariamu Chaurembo, viongozi waandamizi wa Chama kikuu Cha Ushirika wa wakulima Mtwara-Masasi ( MAMCU) pamoja na wakulima wa zao la korosho wilayani humo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mikakati wa Benki hiyo, Msafiri Shayo alisema kupitia droo hiyo benki ilitoa zawadi za aina mbalimbali zipatazo 19 ikiwemo Guta (Toyo) 1, pikipiki 3, baiskeli 5 na pampu za kupulizia dawa mikorosho 10, kwa wakulima mmoja mmoja pamoja na AMCOS kutoka wilaya hizo ambao waliibuka washindi wa kupitia droo hiyo.

“Mpaka mwisho wa kampeni hii tunategemea kutoa zawadi zenye thamani ya shilingi milioni 150 kutolewa kupitia kampeni hii. Nichukue fursa hii kuwataarifu wakulima na vyama vyote vya msingi kuwa kampeni hii bado inaendelea mpaka katikati ya mwezi Disemba, ambapo tutafanya Droo kubwa ambapo mshindi atajitwalia Treka Mpya kabisa.’’

“Hivyo naendelea kuwasihi wakulima, AMCOS na UNION zote kuendelea kupitisha malipo yao ya korosho Benki ya NBC ili waendelee kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo matrekta’’ alisema Shayo.

Kwa upande wao Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bi Claudia Kitta na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Bi. Mariamu Chaurembo walipongeza aina ya zawadi zinazotolewa kupitia kampeni hiyo kwa kuwa zinalenga kuwakwamua wakulima wa zao korosho mkoani humo kukabiliana na changamoto zinazokwamisha jitihada zao katika kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

“Kimsingi ni kwamba kampeni hii ipo sehemu sahihi kwa wakati sahihi hususani kipindi hiki ambacho sisi kama mkoa tupo kwenye utekelezaji wa mkakati wetu wa kuongeza uzalishaji wa zao la korosho kutoka tani 280,000 zinazozalishwa sasa hadi kufikia tani 700,000 ifikapo mwaka 2025…nawapongeza sana NBC na niwaombe sana wakulima wachangamkie kampeni hii kwa kufungua akaunti zao Benki ya NBC,’’ alisema Bi Kitta.

Aidha viongozi hao waliiomba benki hiyo kuangalia uwezekano wa kuongeza matawi yake ikiwemo huduma ya uwakala wa kibenki katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo ili wakulima hao waweze kunufaika zaidi na huduma hizo zinazoambatana na mikopo ya zana za kilimo na ushauri wa kitaalamu kuhusu kilimo cha kisasa.

“Zaidi pia niwaombe sana wakulima walioshinda zawadi hizi waweze kutumia vifaa hivyo ipasavyo ili viweze kuwasaidia katika kuhakikisha wanaongeza uzalishaji wa zao hili kwa kujiandaa vema kwa ajili ya msimu ujao.’’ Alisema Bi Chaurembo.

Kwa upande wao washindi wa droo hiyo waliishukuru benki ya NBC kwa kuandaa kwa kampeni hiyo kwa kuwa imekuwa na msaada mkubwa kwao.

“Mbali na zawadi mbalimbali ambazo tumefanikiwa kupata kupitia kampeni hii ya Vuna Zaidi na NBC Shambani’’ tunashukuru pia tumepata hamasa na elimu ya kutosha kuhusu kilimo cha zao hili kibiashara zaidi.’’ Alisema Bw Salum Rashid Said, mmoja wa washindi wa Pikipiki kupitia kampeni hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bi Claudia Kitta (wa tatu kushoto) akikabidhi zawadi ya pikipiki ya mataili matatu (Guta) kwa mmoja wa wakulima wa zao la korosho mkoa wa Mtwara Bw Edwin Jackob Amir kutoka CHAMALI Amcos ambae ni mmoja wa washindi wa droo ya pili ya kampeni ya Vuna Zaidi na NBC Shambani inayoendeshwa na Benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara, wakati wa hafla ya ya kukabidhi ya zawadi mbambali kwa washindi wa kampeni hiyo iliyofanyika wilayani Masasi mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Bi. Mariamu Chaurembo (Kulia) pamoja na maofisa kutoka benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Mikakati wa Benki hiyo, Msafiri Shayo (wa pili kushoto)







Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bi Claudia Kitta , Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Bi. Mariamu Chaurembo pamoja na  Mkuu wa Kitengo cha Mikakati wa Benki ya NBC Bw Msafiri Shayo wakikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa droo ya pili ya kampeni ya Vuna Zaidi na NBC Shambani inayoendeshwa na Benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara, wakati wa hafla ya ya kukabidhi ya zawadi mbambali kwa washindi wa kampeni hiyo iliyofanyika wilayani Masasi mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni viongozi waandamizi wa Chama kikuu Cha Ushirika wa wakulima Mtwara-Masasi (MAMCU), viongozi wa chama na serikali pamoja na maofisa kutoka benki hiyo.

Zawadi mbalimbali zilizotolewa kwa washindi wa wa droo ya pili ya kampeni ya Vuna Zaidi na NBC Shambani inayoendeshwa na Benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara.

Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bi Claudia Kitta akizungumza kwenye hafla hiyo.


Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Bi. Mariamu Chaurembo akizungumza kwenye hafla hiyo.



Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo wa Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa akizungumza kwenye hafla hiyo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...