Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameshuhudia shughuli ya kufunga njia, kuchepusha maji na kuanza ujazaji maji kwenye bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHPP).

Mradi huu ulianza mwaka 2018 baada ya Serikali ya Tanzania kupata Kandarasi ya ujenzi ubia wa kampuni ya Arab Contractors na El-Sewedy kutoka Misri.

Rais Samia amesema mradi huu ni mojawapo ya miradi mikubwa ya umeme barani Afrika ambapo bwawa hilo litaweza kuweka akiba kubwa ya maji na kuzalisha umeme hata mvua inapopungua.

Pia Rais Samia amesema mbali na kusaidia kudhibiti mafuriko ya mara kwa mara ya mto Rufiji bwawa hili litawezesha kilimo cha uhakika cha umwagiliaji.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ameagiza Wakuu wa Mikoa kuwazuia wananchi wanaochepusha maji katika maeneo mbalimbali hasa katika Bonde la Mto Rufiji na kurejesha maji katika mikondo yake ya asili kwa kuzingatia kanuni za mgawanyo wa maji.

Vile vile Rais Samia amezitaka Wizara husika kutokutoa vibali vya matumizi ya maji na uwekezaji kwenye shughuli za uzalishaji unaohitaji maji mengi katika maeneo ya juu ya bonde (upstream) na badala yake utumike uwanda wa chini wa mradi.

Kukamilika kwa Mradi wa JNHPP ambao umefikia asilimia 78.68 kutaimarisha na kufungua fursa nyingi za utalii katika eneo la kusini mwa Tanzania hususan katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na hivyo kutoa ajira kwa wananchi.


Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali alipowasili Rufiji mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022 kwa ajili ya kushiriki katika Shughuli ya Kufunga Njia ya Kuchepusha Maji na Kuanza Ujazaji wa Maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) kwenye Mto Rufiji mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais  Mstaafu wa Awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipowasili katika Shughuli ya Kufunga Njia ya Kuchepusha Maji na Kuanza Ujazaji wa Maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) kwenye Mto Rufiji mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza, Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme nchini TANESCO Maharage Chande kuhusiana na jengo la Mitambo (Power House) kwenye Mradi wa Bwawa la kuzalisha umeme (Megawati 2115) la Julius Nyerere JNHPP katika Mto Rufiji tarehe 22 Desemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria Hatua ya Kufunga Njia ya Kuchepusha Maji na Kuanza Ujazaji wa Maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme (Megawati 2115) la Julius Nyerere JNHPP kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na wananchi wa Mikoa ya Pwani na Morogoro kabla ya kuzindua Shughuli ya Kufunga Njia ya Kuchepusha Maji na Kuanza Ujazaji wa Maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme (Megawati 2115)   la Julius Nyerere (JNHPP) kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022.



Wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wakishuhudia Shughuli ya Kufunga Njia ya Kuchepusha Maji na Kuanza Ujazaji wa Maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) kwenye Mto Rufiji mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Mradi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme (Megawati 2115) la Julius Nyerere (JNHPP) kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapatia tuzo Marais Wastaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi pamoja na Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete kutokana na mchango wao katika ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) kwenye Mto Rufiji mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaonesha Marais Wastaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi pamoja na Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson na Waziri wa Nishati Mhe. Januari Makamba  Njia ya kuchepusha Maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme (Megawati 2115)   la Julius Nyerere JNHPP kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...