NA FARIDA MANGUBE. MOROGORO.
TUME ya madini imeandaa kikao kazi cha wakaguzi migodi na baruti nchini ili kuwa na uelewa wa pamoja katika suala zima la usimamizi na uendeshaji wa migodi.
Katika kikao kazi hicho kilichofanyika Mjini Morogoro kimewakutanisha wakaguzi wa migodi na baruti kutoka katika maeneo yote yanayofanywa shughuli za uchimbaji wa madini kwa ngazi zote hapa nchini.
Akizungumza katika kikao kazi hicho Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba amewataka wakaguzi wa migodi na baruti kutumia kikao kazi hicho kama fursa pindi watakapo rudi katika maeneo yao ya kazi kuwaelimisha wachimbaji katika suala zima la utunzaji wa mazingira ili kuepukana na mabadiliko ya tabianchi yaliyoukumba ulimwengu mzima .
Alisema Idadi ya vifo vitokanavyo na ajali maeneo mbalimbali ya migodini hapa nchini imepungua kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma kutoka vifo 106 idadi liyoripotiwa mwaka 2018 hadi kufikia 33 kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni.
“Hapo nyuma matukio ya ajali migodini yalikuwa kwa wingi sana,kwa mwaka 2018 matukio ya ajali ambayo yaliripotiwa yalikuwa 63 na katika matukio hayo vifo vilikuwa ni 106,watu waliopata ulemavu walikuwa 43,tumefanya kazi kubwa ili kuhakikisha matukuo ya ajali na vifo vinapungua”alisema Yahya.
Katibu huyo alimpongeza Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira pamoja na wakaguzi wote wa tume ya madini kwa kitendo cha kuchukua hatua ambayo imeweza kusaidia kupunguza matukio ya ajali na vifo migodini.
Alisema matukio ya ajali midogoni kwa wachimbaji wakubwa na wakati yapo kwa kiasi kidogo tofauti na wachimbaji wadogo wa kwani ndiyo hawanga wakubwa wa ajali hizo na hiyo ni kwa sababu na uduni wa teknolojia wanazozitumia wao.
“Mara nyingi wachimbaji hao hutumia matimba na kwamba matimba hayo yasipopangwa vizuri,kuwa imara,yakitumika muda mrefu huoza na kusababisha mashimo ambayo huwafukia ndugu zetu ambao ni wachimbaji”alisema Yahya.
Aidha alitaka matumizi mazuri ya baruti ili kuepuka kuathiri kwenye jamii zinayozunguka migodi ambapo aliwataka wakaguzi kuhakikisha suala hilo la baruti linatumika vizuri pamoja na kuweka takwimu za matumizi na pia kuhakikisha wote wanaohusika na baruti wanakuwa na vibali.
Kwa upande wake Mkaguzi Mkuu wa Migodi ambaye pia Mkurugenzi wa Ukaguzi Migodi na Mazingira Mhandisi Henri Nditi alisema kuwa semina hiyo itawapa ari na nguvu mpya wakaguzi wa migodi katika kutekeleza majukumu yao.
Alisema kwenye uchimbaji wa madini ili uwe endelevu lazima kuwe salama,kusiwe na ajali na pia mazingira yatunzwe kwa manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadaye na kwamba semina hiyo ni muhimu sana katika kukuza sekta ya madini nchini.
Kwa upande wake mshiriki wa semina hiyo Mhandisi Gabriel Senge alisema katika kikao kazi hicho na mafunzo hayo washiriki wanatarajia kujifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kuendeleza na kusimamia usalama katika migodi,utunzaji wa baruti ili kuongeza tija katika uzalishaji madini.
Kikao kazi hicho kitafanyika kwa siku mbili kimewakutanisha wakaguzi migodi na baruti nchini 63 kutoka katika maeneo yote yanayofanywa shughuli za uchimbaji ili kutoa elimu kwa wachimbaji migodini kutambua umuhimu wa utunzaji wa mazingira, kuimarisha usalama utakao sababisha uchimbaji uendelee kuwanufaisha wachimbaji bila madhara yoyote pamoja na taifa kwa ujumla katika ukusanyaji wa mapato serikalini ili kuwapatia huduma stahiki wananchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...