KADA Mbobevu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Chacha Wambura ameshinda ujumbe wa Halmashauri Kuu kwenye nafasi 20 Tanzania Bara.
Wambura ameyasema hayo kwa njia ya simu kuhusiana na ushindi huo uliopatikana katika uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika kwa siku mbili mjini Dodoma.
Wakati akiomba kura alisema amekuwa ndani ya Chama kwa muda mrefu na kushika nafasi mbalimbali ambazo ameweza kuzimudu kwa uaminifu na na maarifa yake ya kufanya chama kisonge mbele.
Mbali na kuwa Mwana CCM Wambura ni Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa Kampuni ua WAJA Group na kuamini kuwa anatosha kwenye nafasi hiyo.
Amewashukuru Wajumbe kwa kuwa na imani yake katika harakati za kuhakikisha chama hicho kinasonga mbele kwa kuendelea kushika dola.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...