Benki ya Stanbic Tanzania imetangaza dhamira yake ya kuendelea kuiunga mkono serikali katika kutatua changamoto katika sekta ya elimu kwenye mikoa mbalimbali nchini kwa kuchangia katika kuboresha mazingira ya kujifunzia wanafunzi. Hayo yamebainishwa katika hafla ambayo benki hiyo ilitoa msaada wa madawati 140 yenye thamani ya TZS 19.6 milioni kwa Shule ya Sekondari Kerege pamoja na miti 140 ambayo itakabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika siku zijazo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Tehama na operesheni za Benki ya Stanbic – Mussa Ally alisema; ‘’Tuna nia kubwa na kampeni yetu ya Stanbic Madawati Initative ambayo hadi sasa imechangia takribani madawati 1000 kwa shule mbalimbali nchin,i tangu ilipozinduliwa.
Naye Diwani wa kata ya Kerege Saidi Abdullah Ngatipura ameipongeza benki ya Stanbic kwa jitihada zao za kuendelea kusaidia sekta ya elimu na kuwataka wadau wengine kuunga mkono shule nyingine wilayani humo.
Akipokea msaada huo Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Kerege, Kasika Mateko Kasika alisema kuwa, kupitia msaada huo, wanafunzi wa shule hiyo watakuwa na mazingira bora ya kujifunzia, jambo ambalo anatarajia litaongeza ufaulu wao.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wakuu wa wilaya na serikali za mitaa kutoka Wilaya ya Bagamoyo
.jpeg)
Mkuu wa Tehama na operesheni za Benki ya Stanbic, Mussa Ally (Kushoto) akikabidhi moja ya madawati 140 kwa Diwani wa kata ya Kerege Saidi Abdullah Ngatipura (Kulia) kwa ajili ya shule ya sekondari ya Kerege iliyopo Bagamoyo. Hii ni sehemu ya mpango wa benki wa Stanbic Madawati Initative unaoendelea ambao unakusudia kuchangia madawati kwa shule za Serikali mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifuatiwa na upandaji miti, ambao ni sehemu ya kampeni hiyo ukilenga kurejesha mfumo wa ikolojia kwa kupanda mti kwa kila dawati lililotolewa. Pia kwenye picha ni Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Kerege, Kasika Mateko Kasika (Katikati).

Mkuu wa Tehama na operesheni za Benki ya Stanbic, Mussa Ally akipanda mti katika shule ya sekondari Kerege ambapo benki ya Stanbic imekabidhi madawati na miche 140.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...