Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa bodi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Gemma Akilimali leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wananchi wakati wa mkutano wa kupinga ukatili wa kinsia wa siku 16, za kupinga ukatili wa Kijinsia ambayo hufanyika kuanzia Novemba 25, hadi Desemba 10 kila Mwaka.


Amesema ukatili unaofanyika kwenye jamii na ndani kwenye familia ndio unaowadhuru watoto na wanawake ndio unaowanyima haki zao za Msingi.

Kauli mbiu ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kila uhai unathamani, tokomeza Mauaji ya wanawake na watoto.

Ukatili dhidi ya watoto umekuwa ni sehemu ya maisha ya watoto wengi nchini ambapo asilimia nane ya wanawake na watoto wenye umri wa Miaka 15 hadi wanapata ukatili wa Kingono na wanaofanya ukatili huo ni ndugu wa karibu.

Amesema kuwa Kumekuwa na taaarifa za kingono kwenye kwenye sekta ya usafiri hasa kwenye magari ya watoto kwahiyo usalama wa watoto upo hatarini sana hivyo kila mtu awe mstari wa mbele kupinga ukatili wa kijinsi dhidi ya watoto na wanawake.

"Ni jukumu letu Kila mmoja katika jamii ajisikie kuwajibika kumlinda mtoto ili afurahie utoto wake, ujana wake pamoja na kufurahia uzee wake." Amesema Gemma

Akizungumzia kuhusu ufutuliaji wa sheria ya Ngono amesema kuwa watafatilia sheria ya rushwa ya ngono, ambayo inakaribia kwenda kujadiliwa bungeni ambayo inakipengele cha sheria Rushwa ya ngono ni sawa na uhujumu uchumi. Amesema kuwaTakwimu za Jeshi la Polisi zaJanuari hadi Desemba 2021 zinaonesha kulikuwa na kesi 5899 za ubakaji, matukio ya ubakaji 1677 na Matukio ya mimba za utotoni 1114 .

Pia Gemma ameiasa jamii utendaji Kazi kupinga ukatili wa kijinsia, tusiposhirikiana tutakuwa hatufanyi kazi.

Pia amesema kuwa jamii sijionee aibu kukemea matendo ya ukatili wa kijinsia kwani yamefika hadi ngazi ya Familia. Kwa upande wa Wajenzi wa Afrika ya Baadae. Bulders of Future Afrika, Brenda Mgallah amesema kuwa ukatili ni jambo la kukemewa katika jamii hivyo kila mmoja awe mstari wa mbele kupinga ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Serikali ya Mtaa wa Mabibo, amesema kuwa wanashirikia na TGNP kwaajili ya kupinga ukatili wa kijinsia kuanzia ngazi ya mtaa na familia. Pia amesema kuwa wanashirikiana na viongozi wa dini kwaajili ya kutoa elimu makanisani na misikitini ili kupinga ukatili wa kijinsia aidha amesema kuwa wameanzisha mabaraza la kata kwaajili ya kusimamia na kupinga ukatili ya kijinsia maeneo yote yanayoizunguka jamii.
Mwenyekiti wa bodi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Gemma Akilimali akizungumza na vituo vya Taarifa na Maarifa, viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kuhusu taswira halisi ya namna walivyoweza kukabiliana na ukatili wa kijinsia wakati alipokuwa anafanya ufunguzi wa kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya hiyo Leo jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya TGNP Subira Kibiga akimkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufungua maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya TGNP jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkurugenzi wa Shirika la Builders of Future Africa Brenda Mgallah akizungumza namna wanavyoshirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika kutoa Elimu kwa jamii kufungua maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya TGNP jijini Dar es Salaam yaliyoanza Novemba 25 Hadi Desemba 10 mwaka 2022.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Binti Makini Janeth Johnakizungumza kuhusu namna wanavyitoa elimu hasa kwa watoto wa kike waliopo mashuleni namna ya kujitambua na kupambana na masuala ya ukatili wa kijinsia  kufungua maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya TGNP jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe mbalimbali wakichangia mada kwenye maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya TGNP jijini Dar es Salaam yaliyoanza Novemba 25 Hadi Desemba 10 mwaka 2022.
Baadhi ya viongozi kutoka Serikalini, mashirika, vituo vya Taarifa na Maarifa pamoja na Wananchi mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya TGNP jijini Dar es Salaam yaliyoanza Novemba 25 Hadi Desemba 10 mwaka 2022.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Gemma Akilimali akiwa kwenye picha za pamoja na Makundi mbalimbali kama vile viongozi kutoka Serikalini, Mashirika na Taasisi, vituo vya Taarifa na Maarifa pamoja na Wananchi mbalimbali wakiwa wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya TGNP jijini Dar es Salaam yaliyoanza Novemba 25 Hadi Desemba 10 mwaka 2022.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Gemma Akilimali akiwasili kwenye  maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya TGNP jijini Dar es Salaam yaliyoanza Novemba 25 Hadi Desemba 10 mwaka 2022.
Maandamano yakiendelea 
Burudani zikiendelea 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...