Na Mwandishi Wetu Michuzi TV - Gairo
CHAMA
CHA Mapinduzi ( CCM) kupitia Katibu Mkuu wake Daniel Chongolo kimetoa
maelekezo kwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI) kuratibu na kuangalia uwiano wa walimu ili wapelekwe
kwenye maeneo yenye uhitaji.
Kwa mujibu wa Chama hicho takwimu
zilizopo zinaonesha maeneo ya Mjini kuna walimu wengi kuliko maeneo ya
vijijini hivyo ni muhimu kwa TAMISEMI kuweka uwiano sawa wa walimu ili
kuondoa tabaka lililopo ambalo likiachwa litasababisha maeneo ya
Vijijini kuwa na uhaba wa wasomi.
Akizungumza mbele ya wananchi
na Wanachama wa CCM leo Wilayani Gairo mkoani Morogoro Katibu Mkuu wa
Chama hicho,Chongolo amesema Wilaya ya Gairo kunachangamoto ya uhaba wa
walimu lakini kwenye msawazisho ukiangalia mikoa mingine na hasa maeneo
ya mjini bado takwimu zinaonesha kuna walimu wengi.
"Ni lazima
Wizara zinazohusika kwa kuanza na Wizara ya TAMISEMI tufanye mapitio na
kuleta walimu kwenye maeneo yenye uhitaji badala ya kuacha waendelee
kuwepo kwenye maeneo ya Mji. Maeneo yote ya nchi hii yanahitaji huduma
zinazofafana kama ni walimu basi tuweke msawazisho kote ili elimu
itolewe kwa usawia na ulinganifu wa maeneo yote badala ya kutegemea kuwa
na walimu kwenye maeneo ya Mjini na vijiji kukosa, hiyo inatuwekea
tabaka wa upungufu wa wasomi kwenye maeneo ya vijijini.
"Sasa
hivi shule za Serikali zipo kwenye kila eneo hivyo ni lazima tuzifanye
kuwa bora na kimbilio la wananchi kupeleka watoto na kupata mafunzo
kuanzia ngazi ya msngi mpaka sekondara, nitalisimamia na niwahakikishie
Gairo na yenyewe itaongezewa walimu.
"Nimepata taarifa ndani ya
Mkoa wa Morogoro kuna maeneo yanaziada ya walimu wengi tutapitia takwimu
na tutaiagiza TAMISEMI kuratibu zoezi la kutoa walimu kwenye hayo
maeneo kuja kwenye maeneo ambayo hayana walimu , ukiajiriwa na Serikali
lazima ukubali kufanya kazi kwenye eneo lolote kwasababu lengo ni kutoa
huduma na umewekwa ili ukawezeshe hilo ,
Kuhusu matokeo ya Kidato
cha nne , Chongolo amesema yameshuka sana na hiyo inasababu kwani kama
mwanzo walifanya vizuri kwanini mara ya pili wamefanya vibaya ,maana
yake hapo lazima kunachangamoto."Kamisaa Wetu( Mkuu wa Mkoa) haya
matokeo hayavutii wala hayafurahishi ni lazima tuweke mpango wa kupitia
na kujua wapi tumejikwaaa mpaka tumeanza kushuka.
"Ni lazima
tukae chini tupitie wapi tulipojukwaa turekebishe ili twende mbele
tukipandisha kiwango cha ufaulu kwa watoto wetu,tusipowekeza kwa watoto
kwenye elimu tutakuwepo na vijana ambao tija yake kwa nchi yao ni ndogo
hivyo lazima tuwekeze kwa dhati kabisa kwenye elimu kwa vijana wetu,
tuisimamie tukijua tija yake
"Na ninyi wazazi na ndugu wananchi
ni lazima tujue tunawajibu wa kuwalea watoto wetu na kuwawezesha kupata
elimu kwa kuwawekea miundombinu mizuri ya kupata elimu , Serikali
inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imejenga miungdombinu mingi
sana ya elimu , madarasa yaliyojengwa mwaka 2021 na mwaka 2022 ni mengi
sana.
"Kwa hiyo mabilioni ya fedha yameletwa ndani ya Mkoa wa
Morogoro ikiwemo Wilaya ya Gairo na Mkuu wa Wilaya yenu amesema kwamba
mmenufaika na madarasa hayo.Lazima tuweke nguvu kwenye kuwawezesha
watoto wetu ,tusiwatoroshe kwa ajili ya kwenda kwenye mashamba kulima
,tusiwatoroshe kwenda kufuga mifugo ,tuhakikishe wanapata elimu."
Kuhusu
mazingira, Chongolo amewapongeza Wilaya ya Gairo hasa jitihada
zinazochukuliwa na Mkuu wa Wilaya huku akitoa rai kwa wananchi kupanda
miti pembezoni mwa mito ili kuhakikisha mito haipanuki na kuleta madhara
ya mafuriko na bahati nzuri ameona siku za kribuni jitihada za Wilaya
katika kutunza mazingira ikiwa pamoja na kupanda miti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...