Na Janeth Raphael, Michuzi TV -Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeonesha kukerwa na tabia ya baadhi ya viongozi ambao wamepewa dhamana ndani ya Serikali lakini wanatumia muda mwingi kulalamika badala ya kutekeleza majukumu yao, na kutaka wenye tabia hiyo kuacha mara moja.

CCM kupitia Katibu Mkuu wake Daniel Chongolo kimeyasema hayo leo Januari 24,2023 wakati wa hafla fupi ya  mapokezi ya wajumbe wa Sekretarieti mpya ya chama hicho ambao wamepitishwa na Chama hicho hivi karibuni jijini Dar es Salaam na leo wamewasili Dodoma.

Akizingumza zaidi Katibu Mkuu Chongolo amesema pamoja na mambo mengine bado kuna baadhi ya viongozi Serikalini wameendeleza kulalamika badala ya kutekeleza majukumu yao na Chama hakitakuwa tayari kuwafumbia macho viongozi wa aina hiyo.

“Changamoto kubwa tuliyokuwa nayo ndani ya Chama chetu ni kuwepo kwa baadhi ya watumishi ndani ya Serikali kuendelea kulalamika,unamkuta Waziri aliyepewa dhamana ya kutimiza wajibu wake,Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya badala ya kutimiza wajibu wao bado wao wanaendekekeza kulalamika.

“Hii ni aibu mfano unawakuta watumishi wa serikali wanaenda kwenye vyomba vya habari wanawalalamikia watendaji waliopo chini yao kuwa hawasaidii kufanya kazi kwani kitendo hicho kinaonesha wazi kuwa hautoshi ni sawa na Katibu Mkuu kuwalalamikia waliopo chini yake kuwa hawasaidii kazi,  je unawezaje kulalamika wakati unatakiwa kutumia mamlaka uliyo nayo,”amesema Chongolo.

Aidha amesema changamoto nyingine waliyonayo ni kuwepo kwa baadhi ya watumishi waliopewa majukumu lakini  hawajui majukumu ya nafasi walizopewa.Mkuu wa Mkoa badala ya kutimiza wajibu wake anakaa analalamika, ni vema ikafahamika  hatupo kwenye wajibu wa kusikiliza malalamiko tuko kwenye wajibu wa kutenda 

"Kama Waziri umepewa dhamana ya kutumikia unashindwa kutumikia unachelewesha kutimiza malengo.Wananchi wanataka miungdombinu,dawa za mifugo,huduma za kijamii.Wananchi hawataki maneno maneno, kama ni wachimbaji wadogo na wakubwa hawatendedewi haki sawa.

"Kama ni wakandarasi wa ndani na nje hawatendewi haki sawa kwani wasipotendewa sawa sawa watatuonyoshea kidole tukiruhusu wananchi watunyooshee vidole tutakua hatutendi sawa sawa”ameeleza Chongolo na kuongeza " mimi ni Chongolo ila nikiwa hapa mimi ni Katibu Mkuu wa CCM, hivyo sitaki kuona viongozi watakaosababisha maswali mengi kwa Watanzania yasiyokuwa na majibu tunataka vitendo siyo maneneo."

Aidha Chongolo amesema kuhusu Sekretarieti ni kwamba imeaminiwa zaidi kwa ajili ya kuhakikisha inafanya kazi kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili watanzania pamoja na kujibu hoja 

“Chama chochote cha siasa kina kazi ya  kutafuta na kushika dola na kazi ambayo tunayo kwa sasa ni kwa sasa no  kusimamaia dola tuliyopewa na dhamana ya kuishika na wananchi ili ifikapo 2025 tusiende kuulizwa na wananchi.Niwakumbushe mwaka 2019 Chama kilipewa dhamani ya kushika nafasi za Serikali za Mitaa,"amesema Chongolo.

Katika hatua nyingine Chongolo amesema kuwa Wiki hii wanaanza ziara mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kukagua miradi kuanzia ngazi ya shina hivyo amewataka  watendaji wa ngazi za juu kuhakikisha wanatoaushirikiano na watumishi wa ngazi ya chini.

Aidha Chongolo amesema kumekuwepo na changamoto ya kuchekeana na kufumbiana macho katika mambo ya msingi yanayogusa maisha ya watu.“Katika kipindi hiki msitegemee kuwa tutamfumbia macho mtu Moja ya changamoto tuliyonayo ni kuchekeana kwenye mambo ya kweli kuoneana aibu kwa mambo tunayoyafanya."

Kuhusu wajumbe wa sekretarieti ambao wamepokelewa leo Mjini Dodoma mbali ya Katibu Mkuu , wengine ni Anamiringi Macha-Naibu Katibu Mkuu CCM Bara,Mohamed Said Mohamed-Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,Sophia Mjema-Katibu wa Nec Idara ya Itikadi na uenezi,Dkt.Frank Hawassi-Katibu wa Nec Idara ya Uchumi na Fedha ,Mbarouk Nassor Mbarouk-Katibu wa Nec,Idara ya siasa na uhusiano wa kimataifa (SUKI) na Issa Haji Ussi(Gavu)-Katibu wa Nec Idara ya oganaizesheni.



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza kwenye hafla fupi ya mapokezi ya Sekretarieti mpya ya CCM yaliyofanyika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi jijini Dodoma. (PICHA ZOTE NA CCM MAKAO MAKUU)




Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiwa kwenye picha ya pamoja na Wazee wa mkoa wa Dodoma mara baada ya kusimikwa wakati hafla fupi ya mapokezi ya Sekretarieti mpya ya CCM yaliyofanyika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi jijini Dodoma.



Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndugu Annamringi Macha akizungumza kwenye hafla fupi ya mapokezi ya Sekretarieti mpya ya CCM yaliyofanyika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi jijini Dodoma.



Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Zanzibar) Ndugu Mohamed Said Mohamed (Dimwa) akizungumza kwenye hafla fupi ya mapokezi ya Sekretarieti mpya ya CCM yaliyofanyika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi jijini Dodoma.




Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema akizungumza kwenye hafla fupi ya mapokezi ya Sekretarieti mpya ya CCM yaliyofanyika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi jijini Dodoma.

Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza kwenye hafla fupi ya mapokezi ya Sekretarieti mpya ya CCM yaliyofanyika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi jijini Dodoma.

Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni Ndugu Issa haji Ussi (Gavu) akizungumza wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Sekretarieti mpya ya CCM yaliyofanyika Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dodoma Alhaji Kimbisa akizungumza kwenye hafla fupi ya mapokezi ya Sekretarieti mpya ya CCM yaliyofanyika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi jijini Dodoma.




Wanachama na Viongozi Waliohudhuria Mapokezi


Makatibu Wakuu wa Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi Wakiteta jambo wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Sekretarieti mpya ya CCM yaliyofanyika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...