Kampuni ya Bolt inafuraha kukujulisha kuwa LATRA imetoa notisi ya gazeti la serikali namba 7284, la tarehe 30 Disemba 2022 kuhusu mwongozo mpya wa bei za usafiri. LATRA na wadau wengine wakuu katika tasnia hii wamekuwa na mikutano kadhaa, kufuatia kutolewa kwa Agizo la LATRA Na.01/2022, Machi 2022 ambapo LATRA iliweka ukomo wa kamisheni ya 15%.
Bolt
ilikubali kutii agizo hilo kwa muda ili kuonyesha nia njema licha ya
athari mbaya iliyotokana na upunguzaji wa kamisheni kwenye biashara.
Hili lilifanyika ili kuunda fursa ya azimio la makubaliano ili
kuendeleza sekta ya taxi mtandao nchini Tanzania.
Akizungumza
kwenye taarifa hiyo Meneja wa Bolt Ukanda wa Afrika Mashariki, Kenneth
Micah, alisema “tunapenda kuwashukuru LATRA na mamlaka zinazohusika
ambazo zimefanya kazi bila kuchoka kuhakikisha kuwa kero zilizotolewa na
wadau wa tasnia zinashughulikiwa, ili kuhakikisha hali ya mafanikio kwa
wadau wote”.
Kwa kuzingatia kanuni mpya za LATRA kwa wahusika wa
tasnia ya taxi mtandao, Bolt itafanya mabadiliko kwenye kamisheni
pamoja na nauli kulingana na mwongozo mpya wa LATRA.
Bolt
itaendelea kutoa huduma ya uhakika kwa mamia na maelfu ya watumiaji
Tanzania Bara, ili waendelee kupata njia nafuu, salama na rahisi ya
kuzunguka mjini. Pia tutahakikisha kuwa maelfu ya madereva wanaoendesha
kwenye jukwaa la Bolt nchini Tanzania, wanaendelea kupata fursa za
mapato.
Bolt itaendelea kushirikiana zaidi na LATRA pamoja na
wadau wengine wa tasnia hii, ili kuhakikisha ukuaji wa soko huria na
zuri la huduma za usafiri wa taxi mtandao nchini Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...