Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
KOCHA Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira (Robertinho) imeelezwa kuwa ameondoka kuelekea kwao Brazil usiku wa kuamkia Januari 24, 2023 kwa shughuli binafsi za kifamilia.
Kocha Robertinho ambaye alitangazwa na Simba SC, mapema mwezi Januari imeelezwa kuwa atarejea nchini Tanzania mwishoni mwa mwezi huu ikiwa baada ya kukamilisha shughuli hizo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Simba SC iliyotolewa kupitia mitandao yake ya kijamii imeeleza: “Kocha Mkuu Roberto Oliveira ameondoka usiku huu kwenda nchini kwao Brazil kwa shughuli binafsi za kifamilia na anatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa mwezi huu.”
Wakati huo huo, Simba SC imetangaza ujio wa Klabu ya Al Hilal ya Sudan ambapo Simba SC watakuwa wenyeji wa miamba hiyo ya soka kutoka Sudan. Wekundu wa Msimbazi wamesema kuwa timu hiyo inakuja nchini kuweka kambi ya kujiandaa na michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Klabu ya Al Hilal ya nchini Sudan kesho inatarajiwa kuja nchini kuweka kambi ya kujiandaa na michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba SC tutakuwa wenyeji wao.” Kwa mujibu wa taarifa ya Simba SC.
“Wakiwa nchini watacheza michezo mitatu ya kirafiki dhidi ya Simba SC, Azam FC na Namungo FC. Mchezo wetu dhidi ya Al Hilal utakuwa wa mwisho na utachezwa Februari 5, 2023 kwenye Uwanja wa Mkapa.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...