MBUNGE wa Jimbo la Mlimba mkoani Morogoro, Godwin Kunambi ameipa siku moja Bodi ya Maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kuhakikisha inawarudishia maji wananchi wote ambao walikua wamewakatia maji.

Kunambi ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi katika Kata ya Mchombe ambapo wananchi hao walimueleza changamoto yao hiyo ya kukatiwa maji bila sababu ya msingi.

Kunambi amesema ni makosa kwa Bodi hiyo ya Maji kuwakatia maji wananchi bila sababu yoyote kwa muda mrefu jambo ambalo ni hatari kwa afya za wananchi hao.

" Nimepokea changamoto hii kubwa ya kukatiwa maji kwa wananchi wangu, na siyo hapa Kata ya Mchombe pekee bali wananchi wengi wa Jimbo la Mlimba wanalalamika kukatiwa maji kwa siku zaidi ya tatu, niiagize Bodi ya Maji kuhakikisha ndani ya masaa 24 wanarudisha maji.

Bodi ya Maji mnatakiwa kutoa elimu kwa wananchi wetu kama kuna changamoto yoyote na siyo kuwakatia maji hovyo wananchi wetu, mbaya zaidi mnakata maji kwenye maeneo ambayo yana mkusanyiko mkubwa kama Sokoni huku ni kuhatarisha pia afya za wananchi wetu," Amesema Kunambi.

Akizungumzia sekta ya elimu, Kunambi amesema ndani ya miaka miwili ya uongozi wake amefanikisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ngai ndani ya Kata hiyo na kufanya jumla ya Shule hizo kuwa mbili.

" Wakati tunaingia madarakani tulikuta Kata hii ya Mchombe ina shule moja ya Sekondari ya Nakaguru, lakini ndani ya miaka miwili tunaishukuru Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutuwezesha kuwa na Shule nyingine ya Sekondari," Amesema Kunambi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...