Msingi wa awamu ya nne kutoka Tabora mpaka Isaka unakuja baada ya awamu ya kwanza, pili na tatu ya reli ya Dar es Salaam – Mwanza. Reli hii itakuwa ndefu zaidi kujenga na kampuni jkandarasi ya Uturuki na haraka zaidi ndani ya Afrika Mashariki. TRC imeiambia Yapi Merkezi kuweka mipango ya kukamilisha mradi wa kujenga reli ndani ya miezi 42 kutoka January 2023.
Miundombinu muhimu inataajiwa kuwekwa wakati wa utekelezaji mradi. Yapi Merkezi imechukua jukumu la kujenga vituo vitatu katikati ya miji ya Tabora na Isaka, kituo cha marekebisho, eneo la mizigo, jengo la utawala, taasisi ya reli, reli yenye urefu wa Kilomita 165, mifumo ya alama za mawasiliano na umeme.
Makamu wa Rais Dr Philip Isdor Mpango, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa, Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania. Masanja K Kadogosa, Hakan Alkan na Erhan Cengiz, Makamu Wakurugeni wa Yapi Merkezi Construction, walihudhuria uzinduzi wa ujenzi uliofanyika mjini Isaka Januari, 18, 2023.
Katika hotuba yake Makamu wa Rais alisema, “ Mradi huu wa SGR ni muhimu katika mkakati wa maendeleo ya Tanzania. Zaidi ya fursa 20,000 za ajira zimetengenezwa na jumla ya shillingi trilioni 1.9 za Kitanzania zimekwenda kwa wakandarasi wadogo, ambao wamelipa kodi zinazo kuza pato la taifa”.
Makamu wa Rais aliendelea kwa kupongeza TRC kwa juhudi zao za kuongeza thamani ya pesa kwa wakandarasi wakubwa na wadogo.
“Nina wasihi wakandarasi kufanya kazi kwa uadilifu na kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati” alimalizia.
Naye Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mh. Prof Makame M. Mbarawa, alipongeza TRC kwa ushirikiano na mwongozo inaouonyesha katika mradi wa SGR na kuuhakikishia umma kwamba serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasan imedhamiria kuwekeza katika miundombinu ya usafiri ili kuimarisha mifumo ya usafiri inayokwenda kukuza uchumi wa taifa. Waziri alisema kuwa takribani asilimia 14 ya pato la taifa imeongezeka kutoka na shughuli za usafirishahi bidhaa, huduma na watu.
Yapi Merkezi imetekeleza kwa umahiri miradi yake ya nyuma iliyofanyika nchi mbalimbali duniani na awamu ya nne ni matokeo ya ukamilishaji mzuri wa awamu mbili za kwanza za mradi wa SGR Tanzania.
Kampuni hiyo imefanikisha kikamilifu shughuli zote awamu ya tatu mwezi Disemba 2021 kutokana na mafanikio ya awamu mbili za mwanzo wa mradi.
Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa awamu ya nne yenye urefu wa takribani km 165, Hana Alkan, Naibu Meneja Mkuu wa Yapi Merkezi Construction, alisema “Leo, tunafuraha kuongeza mradi mmoja mwingine tuliofanikisha kuufanya barani Afrika. Uongozi wa shirika la reli Tanzania umetuzawadia awamu ya tatu na ya nne ya reli hii ya muhimu kutokana na uadilifu wetu na ubora wa kazi tuliouonyesha katika vipande vya reli viwili vya kwanza, Dar es Salaam-Mwanza chenye urefy wa km 722 kutoka Dar es Salaam mpaka Makutupora, ambacho ni kipande kirefu zaidi cha reli, kuwahi kujenga na kampuni ya Kituruki barani Afrika na chenye mwendo mkali zaidi Afrika Mashariki.
Pia Mkurugenzi wa TRC Masanja K. Kadogosa alisema “ SGR itapunguza muda uliokuwa ukipotea kusafirisha bidhaa, huduma na watu, jambo litakalo punguza gharama za usafirishaji bidhaa na huduma pia. Kwa mfano, itachukua takribani masaa 8 kusafiri kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza. Vile vile mradi utafaidisha wakazi wa maeneo ya miji ambapo mradi unafanyika.
Makamu Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Philip Isdor Mpango akiangalia na kusikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa shirika la reli (TRC) Masanja K Kadogosa kuhusu reli ya kisasa ya SGR inayojengwa na kampuni ya Uturuki ya Yapi Merkezi katika kipande kinachojengwa cha Tabora-Isaka kilichozinduliwa mjini Isaka, Jumatano.
Wakazi wa mji wa Isaka wakifurahia uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR uliofanyika mjini humo Jumatano. Reli ya SGR inajengwa na kampuni ya Uturuki ya Yapi Merkezi.
Shirika la Reli la Tanzania (TRC) limedhamiria kuboresha usafiri wa reli na kubadilisha Maisha ya wasafiri nchini. Jambo hilo litapunguza gharama za usafiri.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...