Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Azam FC wapo mguu mmoja ndani, mguu mwingine nje ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi 2023 baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Malindi SC kwenye mchezo wa Kundi A uliopigwa kwenye dimba la Amaan visiwani Zanzibar.
Azam FC walianza kupata bao kwenye dakika ya 33’ kupitia kwa Mshambuliaji wao, Ayoub Reuben Lyanda, huku bao la kusawazisha la Malindi SC likifungwa na Mshambuliaji wa timu hiyo, Said Omar Natepe akiunganisha ‘krosi’ safi ya Mohamed Mussa kwenye dakika ya 77’.
Msimamo wa Kundi A la mashindano hayo, Malindi wanashika usukani kwa alama zao nne huku Azam FC wakiwa nafasi ya pili wakiwa na alama moja pekee wakati Jamhuri ya Pemba ikiwa haina alama yoyote.
Azam FC watalazimika kupata ushindi wa zaidi ya mabao mawili katika mchezo wao dhidi ya Jamhuri ya Pemba ili kujihakikishia nafasi ya kwanza ya msimamo wakifika alama nne sawa na Malindi ambao wanaongoza Kundi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...