Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
WANACHAMA
zaidi ya 250 wa Chama Cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA)
wanatarajia kushiriki kwenye mkutano Mkuu wa Chama hicho utakaofanyika
hapo kesho Jumamosi jijini Dar es Salaam, ambapo Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa atakuwa mgeni rasmi.
Akizungumza
na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaamu,Mwenyekiti wa TATOA amesema
kuwa mkutano wao wa Saba wa mwaka utafanyika katika Hoteli ya Johari
Rotana na madhumuni ya mkutano huo ni kuwaleta wasafirishaji wote wa
sekta ya uchukuzi pamoja ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana
na sekta ya usafirshaji.
"Hii inajumuisha changamoto zote zinazoikabili
sekta
ya usafirishaji. Mkutano huo utajumuisha wadhamini ambao watakuwa
wakiwasilisha,kuonesha bidhaa na huduma zao ambazo zinaongeza utendaji
kazi katika sekta ya usafirishaji..
"Wadhamini hao kwa pamoja ni
Total Energies, benki ya NBC, Double Click, UTrack, GF trucks &
equipment na korridor. TATOA ni chama cha hiari cha wafanya biashara
yakusafirisha mizigo kwa njia ya barabara ndani na nje ya Tanzania,
hususani katika nchi zilizo katika kanda ya jumuiya ya kusini wa Afrika
(SADC).
"Na jumuiya ya AfrikaMashariki (EAC).DRC (Katanga, Mikoa
ya Kivu ya Kaskazini na Kusini), Zambia, Malawi,Zimbabwe, Rwanda,
Burundi, Uganda, naSudan Kusini. Ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na
wanachama 25 pekee.TATOA imekua na kuwa chama cha wafanyabiashara
waliojitolea ambao wanaona sekta ndogo ya usafirishaji wa barabara
inakuwa mchangiaji namba 2 wa Pato la Taifa kuwa na wanachama zaidi ya
900," alisema Lukumay .
Aidha Lukumay alifafanua kuwa Mkutano
Mkuu wa 7 wa Mwaka wa TATOA unatarajia kuhudhuriwa zaidi ya Wanachama
250 ambao ni wamiliki wa kampuniza usafirishaji . Wafadhili kutoka
Totalengies, Benki ya NBC, Doubleclick-U-track, GFtrucks and equipment,
korridor watatoa suluhisho ya mambo mbali mbali yanayohusiana na sekta ,
hiyo ni kupitia maonesho ya bidhaa pamoja na huduma wanazotoa.
Kwa
upande wake Meneja Masoko na Mawasiliano wa GF Trucks and Equipment,
Smart Deus, aliwahimiza wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi
katika mkutano huo huku akieleza kuwa wana ofa mbalimbali kwa ajili ya
wateja wao.
"Katika mkutano huo tutatangaza kampeni maalum ya kutoa
huduma za kiufundi bila malipo kwa malori yanayopita katika Barabara kuu
ya Morogoro kwenda nchi jirani," Alisema Deus.
Katika hatua
nyingine Meneja wa kitengo cha vilainishi kutoka Total Energies, Ally
Saleh amesema kampuni hiyo imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na TATO.
"Kwetu
sisi wasafirishaji ni wengi kuliko wateja kwa sababu licha ya kununua
mafuta na mafuta kutoka kwetu tunawafuatilia ili kuhakikisha vifaa vyao
vinafanya kazi ipasavyo na kwa ufanisi," alisema Salehe
Mgeni
rasmi katika mkutano huo atakuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof
Makame Mbarawa na wakuu wa mashirika mbalimbali ya serikali ikiwemo,TPA,
TRA, LATRA, EWURA, TANROADS, GCLA, TASAC. Wanachama pia watapata fursa
ya kuunganishwana wanachama wengine kutoka katika sekta hiyo
ya usafirishaji.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), Elias Lukumay
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano mkuu wa
mwaka kujadili changamoto utakaofanyika jijini Dar es Salaama
kesho.Kulia ni Meneja masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks
& Equipments Ltd Smart Deusi na katikati ni Mkurugenzi mwendeshaji
wa kampuni ya Double luck consulting ltd, Sandeep Basra na kushoto ni
Meneja wa kampuni ya Total Energies, Ally Saleh
Meneja
wa kampuni ya Total Energies, Ally Saleh akizungumza na wandishi wa habari
kuhusu maandalizi ya mkutano mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Malori
Tanzania (TATOA) kujadili changamoto mbali mbali utakaofanyika jijini
Dar es sdalaam kesho.Wengine ni Mwenyekiti wa Chama hicho, Elias Lukumay
, Mkurugenzi mwendeshaji wa kampuni ya Double luck consulting ltd,
Sandeep Basra na kulia ni Meneja masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF
Trucks & Equipment’s Ltd Smart Deusi .
Meneja
Masoko na Mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd,
Smart Deusi akizungumza na wandishi wa habari kuhusu maandalizi ya
mkutano mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) kujadili
changamoto mbalimbali utakaofanyika jijini Dar es sdalaam kesho, Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), Elias
Lukumay na katikati ni Mkurugenzi mwendeshaji wa kampuni ya Double luck
consulting ltd, Sandeep Basra.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), Elias Lukumay
akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano mkuu wa
mwaka kujadili changamoto utakaofanyika jijini Dar es Salaama
kesho Jumamosi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...