Mamlaka ya Uhifadhi Wanyamapori Tanzania Ikiongozwa na Kaimu Kamishna wa Uhifadhi Mabula Nyanda wameitembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro Mhe. Fatma Mwasa kwa lengo la Kujitambulisha, na kumpa taarifa zinazohusu Uhifadhi katika Mkoa huo.

Katika salamu hizo, Kamishna wa Uhifadhi alimpatia taarifa ya shughuli mbalimbali ambazo TAWA inafanya katika Pori Tengefu la Kilombero, Fursa na changamoto pamoja na hatua mbali mbali ambazo TAWA imeshachukua katika kukabiliana nazo.

Aidha Mkuu wa Mkoa Mhe. Fatma Mwasa ameishukuru TAWA kwa kufika ofisini kwake, kumkaribisha vizuri Morogoro, na kuahidi ushirikiano katika masuala mbalimbali yanayohusu Maendeleo.

“Pamoja na jukumu Lenu kubwa la Uhifadhi Wanyamapori, uwepo wa Makao Makuu yenu hapa Morogoro ni wa msingi sana. Kwani vyanzo vya maji vinakauka, Sababu ya wafugaji wavamizi katika maeneo yenye vyanzo vya maji, Ukataji hovyo wa Miti. Zaidi ya watu milioni 11 wanaoishi hapa na maeneo jirani wanategemea maji ambayo vyanzo vyake ni kutoka Morogoro. Nitashangaa sana kama mtaharakisha kuhamia Dodoma wakati bado mkoa wa Morogoro unawahitaji sana.” Alisema Mhe. Fatma Mwasa.

Kamishna wa TAWA alimkabidhi Mkuu wa Mkoa Nembo ya TAWA na Jarida ambalo lina habari za TAWA.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...