
"Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinajivunia mabadiliko makubwa yaliyofikiwa Zanzibar katika kipindi cha miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ambayo yamewafanya wananchi kujiamini na kujiitegemea kimaendeleo" Shaka Hamdu Shaka, Mwenezi CCM Taifa
"Zanzibar imepiga hatua kubwa sana na Chama Cha Mapinduzi inatoa pongezi za dhati kwa kazi kubwa iliyokwishafanywa na inayoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya nane chini ya Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi, ikiendelea kuunga mkono juhudi za kukomesha ukandamizaji wa haki , ubaguzi, Dhulma na manyanyaso"- Shaka Hamdu Shaka, Mwenezi CCM Taifa.
"Katika kipindi cha miaka 59 ya Mapinduzi matukufu licha ya kuleta ukombozi kamili lakini pia yamewafanya wananachi kuwa na fikra huru na kujitawala"
Shaka Hamdu Shaka, Mwenezi CCM Taifa.
"Kabla ya mapinduzi lipo tabaka lilokandamiza, kubagua na kuwapuuza wengine huku wananachi wakikosa haki za msingi na kutotumia fursa za kiuchumi sawa na utu wao kutothaminiwa, na kupuuzwa," Shaka Hamdu Shaka, Mwenezi CCM Taifa
"Mapinduzi ya mwaka 1964 ni ushahidi kuwa Zanzibar ilikuwa na watu waliokoseshwa elimu bora, kutomiliki uchumi, ardhi, kukosa makaazi bora na kunyimwa huduma za jamii" Shaka Hamdu Shaka, Mwenezi CCM Taifa
"Serikali zote SMZ (Serikali ya Mapinduzi Zanzibar) na SMT (Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) zimetimiza wajibu wa kusimamia maendeleo. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais Dk. Mwinyi baada ya miaka 59 wametafsiri mapinduzi ya ukombozi kuwa Mapinduzi ya kiuchumi. Maendeleo yanayoonekana sasa hayakuwepo miaka 200 ya utawala wa kikoloni,"Shaka Hamdu Shaka, Mwenezi CCM Taifa
" Kazi kubwa iliyofanywa na Chama cha ASP ilikuwa kuhakikisha utawala wa ukandamizaji, uonevu na ubaguzi wa huduma za jamii unakomeshwa katika visiwa vya Unguja na Pemba kwa sera ya mapinduzi ya ukombozi na kazi iliyobaki ni kujenga uchumi na maendeleo" Shaka Hamdu Shaka, Mwenezi CCM Taifa
"Ni vyema kwa watendaji waliopewa dhamana katika Serikali na taasisi za umma kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kumsaidia Rais Dk. Mwinyi ili akamilikshe kazi ya kutekeleza mapinduzi ya kiuchumi na kuongeza Kasi ya kuleta maendeleo.” Shaka Hamdu Shaka, Mwenezi CCM Taifa
"Kazi ya kumwondoa mkoloni aliyetawala kwa ubaguzi na ukandamizaji imemalizika. Kazi iliyobaki ni kuongoza kwa haki, umoja na maendeleo. Kukumbuka madhila yaliyokuwepo kabla ya mapinduzi kunatupa ari ya kufikia mabadiliko tuanayoyataka," Shaka Hamdu Shaka, Mwenezi CCM Taifa
"Baada ya kufanikisha mapinduzi ya mwaka 1964 na utawala kushikwa na ASP, Rais wa kwanza wa Zanzibar hayati Mzee Abeid Amani Karume alianza utekelezaji wa sera za maendeleo ikiwemo kutolewa bure kwa huduma za msingi" Shaka Hamdu Shaka, Mwenezi CCM Taifa
"Elimu imetolewa bure, maji safi na matibabu, serikali ikaweka viwango vya mishahara minono kwa mujibu wa ajira ya kila mfanyakazi, yamejengwa makaazi ya kisasa na sasa kazi hiyo inaendelezwa na serikali ya Rais Dk. Mwinyi," Shaka Hamdu Shaka, Mwenezi CCM Taifa
"Ni waombe watanzania wenzangu hasa vijana kutobabaishwa na porojo za baadhi ya wapinga maendeleo na mapinduzi matukufu ya 1964 ambao wamekuwa wapotoshaji wa ukweli kwa kudai serikali za CCM hazijafanya lolote tangu mwaka 1964 wakati asiliamia 98 ya maendeleo yaliyofanyika nchini yamepatikana katika utawala wa Chama Cha Mapinduzi" Shaka Hamdu Shaka, Mwenezi CCM Taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...