Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akizungumza na Maafisa elimu na wakuu wa Wilaya ili kujadili hali ya usaili wa wanafunzi mashuleni katika kikao kilichofanyika Januari 18, 2023. Kulia ni Afisa Elimu Mkoa wa Singida, Maria Lyimo
Na Mwandishi Wetu, Singida.
MAAFISA elimu na Wakuu wa Wilaya Mkoani Singida wametakiwa kutumia muda wa Siku tatu kuanzia leo kuhakikisha hakuna mtoto atakayebaki nyumbani wakati wengine wakiwa shuleni.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba alipokutana na Maafisa elimu na wakuu wa Wilaya ili kujadili hali ya usaili wa wanafunzi mashuleni .
Amesema idadi ya wanafunzi wa Sekondari walioripoti mashuleni ni ndogo ikilinganishwa na uwingi wa madarasa yalijengwa na Serikali hivi karibuni hivyo ni jukumu la Maafisa elimu hao kuhakisha wanasakwa popote walipo na wapelekwe shuleni.
RC Serukamba ameendelea kueleza kwamba ifikapo Siku ya jumatatu tarehe 23 January 2023 anataka taarifa ya kutoka kila kata kuhusu wanafunzi wangapi wamesajiliwa na wangapi bado na Sababu za kutosajiliwa.
Aidha, ametoa wito kwa wazazi na walezi Mkoani Singida kuhakikisha hakuna Mtoto aliyechaguliwa kujiunga na kidato Cha kwanza atakayebaki nyumbani.
"Nimejiridhisha kwamba hali ya usaiili wa wanafunzi wa kidato Cha kwanza inasuasua Sana ,Serikali imejenga madarasa ya kutosha,imefuta Ada mashuleni lakini bado wapo wazazi hawawapeleki watoto wao shuleni hili halitakubalika" Serukamba.
Kwa upande wake DC wa Iramba Suleimani Mwenda amesema bado Katika Wilaya yake bado hali ya kujiunga na kidato Cha kwanza unaenda kwa kusuansua Jambo ambalo waliamua kuchukua hatua kwa kuwaita wazazi na wanafunzi ofsini kwake ili kuwasikiliza.
DC Mwenda anasema amebaini kwamba wapo wazazi wanaozuia watoto kwenda shule ili waweze kujiunga na Shughuli za kiuchumi za kulima kuchunga mifugo na bĂ adhi Kutafuta ajira binafsi.
Mwenda amesema wanapenda kutumia mbinu zote zikiwemo kuwashawishi kutumia Dola kuwapeleka shule na kuwachukulia hatua wazazi Watakao bainika kuwazuia watoto kwenda shule.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akikisisitiza jambo kwenye kikao hicho
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Ikungi, Margaret Kapolesya akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...