Na Pamela Mollel,SERENGETI
Hifadhi ya Taifa Serengeti imetembelewa na Spika wa Bunge la India, Mhe. Om Birla ambaye ni mtu maarufu Dunia ikiwa ni sehemu ya mapumziko pamoja na kujionea vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika Hifadhi hiyo iliyojaliwa vivutio lukuki
Akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Seronera mara baada ya mapokezi hayo Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Mkuu wa Kanda ya Magharibi TANAPA, Martin Loibooki alisema ujio wa Spika ni fursa kubwa katika kutangaza Hifadhi hiyo maarufu Dunia
Alisema kuwa wao wanajivunia na kuona fahari ujio wa Spika wa Bunge la India pamoja na timu yake itasaidia sanaaa kutangaza Hifadhi
"Spika ni mtu maarufu nani kiongozi mkubwa nchini kwao, ujio wake katika Hifadhi ya Taifa Serengeti utasaidia kuendelea kuitangaza Hifadhi hii na kufanya wageni wengine mashuhuri kutembelea lakini pia watalii kutoka Taifa la India"alisema Loibooki
Kwa upande wake Upendo Massawe, ambaye ni Afisa Mhifadhi Mkuu na Msimamizi wa Idara ya Utalii, Serengeti amebainisha kwamba Hifadhi ya Taifa Serengeti ni kati ya Hifadhi maarufu Dunia na wamejidhatiti katika vilivyo kuhakikisha wageni wote wanaotembelea wanafurahia vivutio vinavyopatikana katika Hifadhi
Hifadhi ya Taifa Serengeti ni ya kwanza kuanzishwa nchini Tanzania iliyojizolea umaarufu zaidi ulimwenguni kwa kutembelewa na wageni mashuhuri Duniani.
Wapili kulia ni Naibu Kamshna wa Uhifadhi na Mkuu wa Kanda ya Magharibi TANAPA, Martin Loibooki akipokea ujio wa Spika wa Bunge la India Mhe.Om Birla na timu yake katika uwanja wa Seronera uliopo katika Hifadhi ya Serengeti
Afisa Mhifadhi Mkuu na msimamizi wa idara ya utalii Serengeti Upendo Massawe akizungumza na vyombo vya habari juu ya ujio wa Spika wa bunge la India
Afisa Mhifadhi Mkuu na msimamizi wa idara ya utalii Serengeti Upendo Massawe akizungumza na vyombo vya habari juu ya ujio wa Spika wa bunge la India
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...