Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Shirikisho la Soka nchini (TFF) limeishutumu Klabu ya Gwambina ya Misungwi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kusema uongo kupitia Chombo cha Habari cha Clouds wakidaiwa kutoa shutuma hizo dhidi ya Shirikisho hilo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho hilo, imeeleza kuwa imewaelekeza Wanasheria wake kuchukua hatua dhidi ya Mmiliki wa Klabu hiyo, Alexander Mnyeti na Kituo cha Redio cha Clouds, baada ya Mnyeti kunukuliwa kupitia Kituo hicho kuwa alidaiwa kutoa kiasi cha fedha Tsh. Milioni 5 na Shirikisho hilo ili wapate kibali cha kutumia uwanja wao wa nyumbani uliopo Misungwi.
TFF imedai Gwambina FC kabla ya kujitoa ilikuwa inacheza Ligi Daraja la Pili (First League) wakati ikitumia uwanja wao wa nyumbani ambao upo Misungwi mkoani Mwanza, TFF imedai kuwa wakati huo uwanja huo wa Gwambina FC ulifungiwa kwa kutokidhi vigezo.
Hata hivyo, TFF imevikumbusha Vyombo vya Habari nchini kufuata na kuzingatia misingi ya Taaluma hiyo ikiwemo kutoa taarifa kama hizo bila upendeleo na kushirikisha pande zote mbili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...