Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
WATU watano wamefariki na wengine 10 kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster na gari la mizigo aina ya Mitsubishi Canter.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani ACP Pius Lutumo alisema ,ajali hiyo ilitokea Januari 8 mwaka huu majira ya saa 1:40 asubuhi eneo la Mwavi kata ya Kiwangwa Wilayani Bagamoyo ambapo watu watano wamefariki eneo la ajali huku 10 wakijeruhiwa.
Alisema kuwa basi hilo dogo lenye namba za usajili T 972 DCY lililokuwa likitoka Bagamoyo kwenda Morogoro liligongana na lori dogo lenye namba za usajili T 168 CAZ.
"Katika ajali hiyo waliofariki wanawake wawili na wanaume watatu ambapo majina yao bado hayajafahamika ambapo maiti na majeruhi wako hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo,"alisema Lutumo.
Chanzo cha ajali Coaster lilikuwa linapita gari lingine bila tahadhari na kugongana na gari lingine kusababisha ajali hiyo.
"Madereva wanapaswa kuchukua tahadhari ili kuepuka ajali zisizo za lazima kwa kufuata sheria bila shuruti kwa kuzingatia usalama wao na wengine,"alisema Lutumo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...