Na Janeth Raphael - Kondoa Dodoma

Serikali amewataka wazazi kushirikiana na serikali katika ujenzi na uhifadhi wa Miundombinu ya elimu.

Hayo yamebainishwa leo Januari 27, 2023 na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt Fatma Maganga katika mkutano wa uhamasishaji wa program ya shule bora kwa wasimamizi wa vyombo vya habari na wahariri yaliyofanyika Wilayani kondoa mkoani Dodoma.

Dkt Maganga amesema mkoa wa Dodoma kuna upungufu wa vyumba vya madarasa 7000 ,ambapo mwaka huu 2023 peke yake wanatarajia zaidi ya wanafunzi elfu 90 kuanza masomo.

Dkt Fatuma amesema kuwa swala la Elimu katika Mkoa wa Dodoma bado halijatangazwa vizuri na kuwataka waandishi wa habari wakawe chachu cha kuielimisha jamii.

Amempongeza kwa kusema Rais Samia Sulluh Hassan Kwa jitihada zake za dhati za kuongeza pesa za maendeleo katika mkoa wa Dodoma ambapo shilingi bilioni 7.8 zimetolewa na kuwezesha kujenga vyumba vya madarasa 393 ya shule za msingi na madarasa 130 yamejengwa Kwa shule za kwa gharama ya shilingi bilioni 20

Aidha amewaeleza waandishi wa habari kuwa Rais Samia ameongeza bajeti ya Elimu bila malipo Kwa shule za misingi na sekondari.

Dkt Maganga amewaomba wazazi kuwapeleka watoto wao shule na kuacha tabia kuwafungia ndani
"Ninawaomba wazazi wawapeleke watoto shule ,wasiwafiche na kuwatumikisha Shughuli za kilimo na kazi za ndani."Amesema Dkt Fatuma

Aidha amekemea dhana iliyozoeleka kwamba Mkoa wa Dodoma ni zao la wadada wa ndani kutoa House girl[Wasaidizi wa Shughuli za ndani

Amesema Mpaka kufikia January 26.2023 ilifikia asilimia 89.7 ya wanafunzi wa madarasa la awali walioripoti shule,huku asilimia 94.2 Kwa darasa la kwanza na asilimia 66.95 kidato Cha kwanza

.."Nawaomba waandishi wa habari mkausaidie mkoa kutangaza mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu mkoani kwetu,kuyatangaza mafanikio haya Kwa jamii yatarahisisha serikali kuendelea kutuunga Mkono katika jitihada zetu hizi."Alisema Fatuma

Dkt Fatuma akapongeza kwa kusema juu ya Matamanio ya mkoa ya mwaka huu 2023 ni kuwa na ufaulu wa asili 95 ya matokeo ya mtihani wa darasa la saba na angalau asilimia 75 ya wanafunzi wanaohitimu kidato Cha Nne Wawe na ufaulu wa daraja la 1-3.

"Aidha ni matamanio ya mkoa kuondoa changamoto ya watoto kukaa chini Pamoja na wanafunzi wote watakaoshindwa mtihani wao wa darasa la saba kujiunga na vyuo vya ugundi stadi VETA"Amesema Dkt Fatuma

Kwa upande wake mratibu wa Program ya shule Bora Mkoa wa Dodoma Mtemi Zombwe amesema program ya shule bora inateleleza katika mikoa tisa Halimashauri 67, shule 5,757.

Zombwe ametaja Mikoa hiyo kuwa ni Dodoma, katavi, Kigoma, Mara, Pwani, Rukwa, Simiyu, Singida na Tanga.

Mratibu huyo ametoa wito kwa wandishi wa habari kufanya kazi kwa kufuata Dira nne za Program zilizopo Katika shule Bora

Hata hivyo Zombwe amesema watoto wa darasa la kwanza na lapili ili waweze kufikia malengo ya kujua kusoma na kuandika inahitajika amani kwakua anakua Katika umri mdogo hivyo linalohitajika nikupewa amani

Sambamba na hayo Mratibu huyo ametaja malengo makhususi manne[4] ya Programu hiyo ambayo ni Pamoja na÷


•Kuboresha ujifuzaji

•Kuboresha Ufundishaji

•Kuimairisha Ujumuishi

•Kuimarisha Mifumo.
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt Fatma Maganga akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Mratibu wa program ya shule bora Mkoa wa Dodoma Mtemi Zombwe akingumza na wanahabari na wahariri katika mkutano huo wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mafunzo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...