Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV 

Mshambuliaji raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Lobi Manzoki amedai kuwa baadhi ya watu wenye roho mbaya walimzuia yeye asisajiliwe na Simba SC ya Tanzania, baada ya timu hiyo kuonyesha nia ya kumsajili akiwa katika Klabu ya Vipers ya Uganda.

Manzoki amesema hayo katika Mkutano Mkuu wa Klabu hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam, wakati yeye akihudhuria kama mgeni mualikwa. Hata hivyo, Manzoki ameahidi ndoto yake siku moja kuitumikia Simba SC kwa kuwa anaipenda timu hiyo.

“Watu wenye roho mbaya hawakutaka mimi kucheza Simba SC, mimi binafsi nawaahidi mimi ni Mwanasimba na kama kuna Klabu ambayo ninaweza kucheza barani Afrika ni Simba SC,” amesema Lobi Manzoki alipozungumza mbele ya hadhara ya Mkutano huo.

“Sisi ni vijana lakini muda wetu wa kucheza soka ni mfupi sana, napenda kuwaahidi Simba SC, mimi naamini siku moja tunaweza kuwa pamoja kwa kuwa mapenzi yangu na ninyi ni makubwa sana”, ameeleza Manzoki.

Mara ya mwisho, licha ya kuhusishwa kusajiliwa na Simba SC, Mshambuliaji Lobi Manzoki alihama kutoka Klabu ya Vipers ya Uganda na kusajiliwa katika Klabu ya Dalian Professional ya China. Nyota huyo mwenye asili ya DR Congo  aliwahi kucheza pia AS Vita ya nchini humo na AS Maniema Union ya huko huko.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...