NA SALMA AMOUR, TANGA.
Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya mkinga lapitisha Kwa kauli moja makisio ya mpango na bajeti ya halmashauri Kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 jumla ya shilingi 26,998,507,369 kwa utekelezwaji wa miradi ya maendeleo,ruzuru ya mishahara na matumizi wa kawaida.
Makisio hayo yalipitishwa katika mkutano maalum wa Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya mkinga uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Akiwasilisha rasimu ya makisio ya mipango na bajeti ya halmashauri hiyo kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 mkurugenzi wa halmashauri wilaya ya mkinga Zahra msangi alieleza kuwa ni jumla ya shilingi 26,998,507,369 ambapo kati ya fedha hizo tsh 2,601,959,485 ni mapato ya ndani, shilingi 14,902,856,000, shilingi 869,919,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 8,623,772,884 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa upande Wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya mkinga Abdallah sengano alimpongeza Rais Samia suluhu Hassan kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii hususan katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Shule na vyumba vya madarasa katika Shule za msingi ambapo mpaka sasa serikali inaendelea kutoa fedha.
Katika hatua nyingine kaimu katibu tawala wilaya ya mkinga Erick Farahami alieleza kuwa lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuona Mabadiliko mpaka 2025 ikiwa imeweka mikakati madhubuti ya kuleta maendeleo ya nchi.
"Ni kuwa Rais wetu samia suluhu Hassan anafanya kazi kwa juhudi na uzalendo kwenye Taifa letu lakini ni kuwa anatoa fedha nyingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara,ujenzi wa madarasa,nyumba za wakurugenzi ikiwemo katika halmashauri yetu ya wilaya ya mkinga hivyo niwaombe madiwani wote kumisamia shuhuri za kiserikali ikiwemo ukusanyaji wa mapato Ili kumsaidia Rais Samia katika kufikia lengo husika". Alisema Eric Farahami
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...