Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia promosheni ya bia yake ya Pilsner Lager ijulikanayo kama ‘Kapu la Wana’ imekabidhi zawadi kwa washindi 7 wa droo ya kwanza ya promosheni hiyo kutoka mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya. Zawadi hizo ni pamoja na pikipiki, televisheni na simu janja.
Katika washindi
7, washindi 3 walijishindia televisheni, washindi wengine 3
walijishindia simu janja na mmoja alishinda pikipiki. Makabidhiano ya
zawadi hizo yalifanyika kanda ya Ziwa, Kaskazini na Kusini ambapo
promosheni hiyo inafanyika.
Waliojishindia simu janja ni Agatha
Mvwango (Mbeya), Eli Elias (Arusha) na Hassan Joel (Mwanza), washindi 3
wa televisheni ni Justine Mwaipaja (Mbeya), Neema Abdallah (Mwanza) na
Selina Panga (Arusha). Mshindi wa zawadi ya pikipiki ni Neema Mathias
(Mwanza).
Akizungumza kwenye makabidhiano ya pikipiki kwa mmoja
wa washindi wa promosheni ya ‘Kapu la Wana’, yaliyofanyika Spears Bar
eneo la Magu jijini Mwanza Meneja Masoko wa SBL kanda ya Ziwa, Ronald
Lyatuu alimpongeza mshindi wa pikipiki na kusema kuwa promosheni hiyo
ilianzishwa kwa dhumuni la kuwawezesha wanywaji wa bia hiyo ambao ni
wachapa kazi kwa kuwapa zawadi mbalimbali baada ya kushiriki kwenye
promosheni hiyo, “hii ni mara ya pili tunafanya promosheni hii na
kupitia promosheni hii tunataka kuwapa wateja wetu nafasi ya kuboresha
maisha yao kwa namna moja au nyingine, kwa mfano mshindi wa hii pikipiki
anaweza kuamua kutumia pikipiki hii kumuongozea kipato au vyovyote
atakavyoamua kulingana na mahitaji yake.”
Alitoa wito kwa
wanywaji wa bia hiyo walio kanda ya Ziwa, Kusini na Kaskazini kuendelea
kushiriki kwenye promosheni hiyo na kuwa kwenye nafasi ya kujishindia
zawadi mbalimbali kupitiia promosheni hiyo itakayofanyika kwa muda wa
wiki 8. Promosheni hiyo iliyozinduliwa Februari 02 itatoa zawadi za simu
janja, televisheni, pikipiki na zawadi ya gari kutolea mwishoni mwa
promosheni.
Akielezea jinsi ya kushiriki, Marando alisema, “mteja
atahitaji kununua bia ya Pilsner, halafu atapata kadi ya kukwangu,
ikwangue, kama zawadi ni bidhaa kama fulana, kofia, n.k utazawadiwa
papo hapo na kama zawadi uliyoikwangua ni nambari maalum, itume kupitia
ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwa namba 15320 mfano: Andika Kapu 4321
Iringa (Acha nafasi. Utapokea ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kudhibitisha
ushiriki wako.”
Kwa upande wake, mshindi wa pikipiki, Neema
Mathias alishukuru SBL na kuwapongeza kwa kuandaa promosheni ya ‘Kapu la
Wana’ ambayo ni maalum kwa kuwawezesha watanzania wanaotaka kuboresha
maisha yao, “nimefurahi sana kuwa mshindi wa hii pikipiki, natarajia
kuitumia inisaidie kujiongezea kipato, nawashukuru sana SBL kwa
kutuletea promosheni hii kwani kupitia zawadi hii naamini naenda
kubadilisha maisha yang una familia yangu kiuchumi.”
Kwa upande
wa washindi wa mkoa wa Arusha, makabidihianao ya zawadi za simu janja na
televisheni yalifanyikia Kili Time Bar, eneo la Ngusero. Na kwa
washindi kwa Mbeya, makabidhiano ya zawadi za televisheni na simu janja
yalifanyikia Kiteputepu Bar, iliyopo eneo la Roma Kyela mjini.
Hii
ni mara ya pili bia ya Pilsner imekuja na promosheni hii ya ‘Kapu la
Wana’ na imetenga zaidi ya Tsh. 36 milioni kwa washindi 22 wa kampeni
hiyo.
Washindi wa promosheni ya bia ya Pilsner Lager ijulikanayo kama ‘Kapu la Wana’ inayoendeshawa nakampuni
ya bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL), wakionyesha zawadi zao
wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika mkoani Mwanza siku ya
Jumamosi. Kushoto ni Neema Abdallah, (mshindi wa televisheni), kulia ni
Neema Mathias (mshindi wa pikipiki), wa pili kulia ni Hassan Joel
(mshindi wa simu).Makabidhiano hayo yalifanywa na Meneja Masoko wa SBL
kanda ya Ziwa, Ronald Lyatuu (wa pili kushoto).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...