Na Mwandishi Wetu Michuzi TV- Morogoro
KATIBU Mkuu
wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo amesema atakwenda kumwambia Rais
Samia Suluhu Hassan hakuna chochote kimefanyika katika kituo cha afya Kinole
mkoani Morogoro na watahakikisha hadi Aprili mwaka huu ujenzi wa kituo hicho
unaanza huku akisema wanataka huduma za afya kwa wananchi isiwe anasa.
Akizungumza
leo Februari 3,2023 na wananchi wa Kinole mkoani Morogoro akiwa kwenye kukagua utekelezaji wa Ilani pamoja na uhai wa
Chama hicho, Chongolo amesema atakwenda kumueleza Rais Samia Suluhu Hassan
kuhusu kituo cha afya Kinole kwa kuwa watu wanahitaji kituo hicho.
“Kwasababu
kutoka hapa kwenda mjini ukiwa na ujauzito ni mateso makubwa , lakini niseme
nilijuaje Kinole kuna shida ya afya , kuna siku nilimuita Waziri wa Afya
ofisini kwangu lakini baada ya kuingia nikaona wameingia na wabunge wengine
wawili akiwemo Mbunge wenu.Nikamuuliza amefuata nini akasema anataka kumuona
Waziri.
“Nilipomuuliza
anataka kusema nini ndipo mbunge wenu akanieleza kuhusu kuongezewa fedha za
Hospitali ya Wilaya ili kukamlisha majengo yote likiwemo la Monchwari pamoja na
miundombinu mingine.Pili akaomba fedha za kituo cha afya Kinole zirudishwe
kwasababu zilishakuja zikaondoshwa na hivyo kituo hakikujengwa, hivyo tukakubaliana na Waziri aende akahangaike na
bajeti ili kituo cha Kinole kipate fedha kwa ajili ya kujenga kituo
hicho,”amesema Chongolo.
Amesema
amepata taarifa tayari eneo kwa ajili ya kujenga kituo hicho lipo baada ya
wananchi kuamua kujitolea hivyo akawahakikishia ndani ya miezi miwili kuanzia sasa
fedha zitakuwa zimefika kwa ajili ya kuanza ujenzi.
“Tunataka
huduma ya afya kwa wananchi isiwe anasa, tunataka akina mama wajifungue bila
mateso , akitoka kujifungua akirudi nyumbani amwambie baba ana hamu ya kurudi
kule, “amesema Chongolo.
Kuhusu elimu, Chongolo amesema bado kuna changamoto ya kupeleka mtoto wa kike kusoma , na jamii inaona kama vile mtoto anayestahili kusoma ni wa kiume peke yake jambo ambalo sio sawa na wenye dhana hiyo hawafanyi vizuri.“Pelekeni watoto wa kike wakasome, tunataka wakuu wa mikoa watoke Kinole.”
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema akiwasalimia wakazi wa Kinole akiwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo.Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ameongozana pia na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi (Gavu) pamoja na Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali ambapo ziara hii ina lengo la Kukagua, Kuhimiza na Kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wakazi wa Kinole, Morogoro Vijijini mkoa wa Morogoro.Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi (Gavu) pamoja na Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali ambapo ziara hii ina lengo la Kukagua, Kuhimiza na Kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025
Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi (Gavu) akiwasalimia wananchi wa Kinole.Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema akisonga ugali kwenye moja ya banda la Mama Lishe katika kijiji cha Kinole,Morogoro Vijijini leo Februari 3,2023 walipofika na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi (Gavu) pamoja na Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali kwenye ziara yao ya siku tisa yenye lengo Kukagua, Kuhimiza na Kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025
Pichani juu (wa pili kulia) Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akiwa na Mbunge wa Jimbo la Morogro Kusini Mashariki Mhe.Hamis Taletale pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi (Gavu) wakipata chakula kwa pamoja katika moja ya banda la Mama Lishe mara baada ya kuzungumza na Wananchi wa Kinole,Morogoro Vijijini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...